Jaji Mkuu wa Misri Adly Mansour |
Jaji
mkuu wa mahakama ya kikatiba nchini Misri Adli Mansour anatarajiwa kuapishwa
kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi kumng'oa madarakani rais
Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini
humo.
Mkuu wa Majeshi ya Misri Generali Abdul Fattah al-Sisi |
Mkuu wa jeshi Generali Abdul
Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika
kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,
ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku
nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Mmoja ya Waandamanaji wakionesha pango lenye kumtaka Rais wa Misri atoke Madarakani |
Waandamanaji walimtuhumu yeye na
chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa
kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood
kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha
nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi
alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo
atachukuwa mamlaka ya rais.
Waandamanaji wakiwa Mtaani wakipinga Utawala wa Rais wa Misri Morsi |
Maelfu ya waandamanaji
wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo
kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana
kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Mtoto akiwa ameshika bendera baada ya kutolewa kwa Rais Morsi Madarakani |
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa
kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa
Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako