Thursday 18 July 2013

P.DIDDY ALIVYOTOA SALAM KWA MADIBA MANDELA

Siku kama ya leo July 18, Muasisi wa mkombozi wa Taifa la Afrika ya Kusini, Tata Nelson Madiba Mandela alizaliwa miaka 95 iliyopita, kwa hiyo leo Mandela anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa Hospital huku afya yake ikiendelea kuimarika.
Kutoka Marekani Rappa kutoka kundi la Bad Boyz Paff Daddy (P. diddy) ametambua mchango wa MANDELA na kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa Mzee Mandela kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha ya Mandela na kuandika maneno haya “Happy Birthday Mr. Mandela!! Thank you for all you have done!!”
Nelson Mandela alizaliwa tarehe 18 July mwaka 1918 na baadae kuwa Rais wa kwanza wa Afrika ya kusini aliyechaguliwa kidemokrasia, alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa za ubaguzi wa rangi “Apartheid” nchini Africa Kusini.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako