Friday 29 November 2013

JACKLYN WOLPER "GAMBE" ATAJA LIST YA WANAUME WAKE


Muingizaji wa filamu nchini,Jacklyn Wolper amesema pamoja na kuwa na mahusiano na wasanii wenzake akiwemo Diamond,Jux. lakini Ally Kiba ndiye msanii pekee aliyemtambulisha kwenye ulimwengue wa mtamu wa mapenzi.
Akiongea na Global Publishers,muingizaji huyo alisema aliachana na Ally Kiba kwasababu ya wanawake wengi walikuwa wakimtamani kimapenzi.
 “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi'Alisema Wolper
“Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.”alisema Wolper
 Vipi kuhusu Jux?
  “Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule
mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,”alisema.
 
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.

Wednesday 27 November 2013

UWANJA WA KOMBE LA DUNIA, 2014 WAANGUKA NA KUUA 3


Watu watatu wamethibitika kufariki baada ya uwanja wa Sao Paulo kuanguka.

Akiongea na vyombo vya habari, msemaji wa polisi katika eneo la Sao Paulo amethibitisha vifo hivyo.

Uwanja huo ambao ulitegemewa kufanyika mechi ya uzinduzi wa michuano ya kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Uwanja huo ulitegemewa kuwa umekamilika mwezi ujao, ili uangaliwe na wataalam kutoka FIFA na uweze kuruhusiwa kutumika kwenye michuano inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa Soka duniani.

Uwanja huo ulianza kujengwa Nov. 2012 kwa gharama ya zaidi ya sh. Bilion 400 za kitanzania, mategemeo ya kukamilika Desemba mwaka 2013.

Uwanja wa Sao Paulo ulikuwa unajengwa kukidhi watu 65,000 watakaokaa na kuangalia mechi.

Rais wa FIFA, Sepp Blatter ameandika kwenywe ukurasa wake wa Tweeter "Nimepatwa na majonzi makubwa kupata taarifa za vifo hivyo vya wafanyakazi waliokuwa wanajenga uwanja huo leo natoa salamu za pole kwa wafiwa na familia zao"
 

MTOTO ARUDISHA PENZI LA TYSON NA MONALISA


NDOA ya mastaa wa filamu Bongo, George Tyson na Yvonney Chery ‘Monalisa’ iliyovunjika kitambo, ilirejewa na uhai wa saa kadhaa katika shughuli ya kumpongeza binti yao mpendwa Sonia baada ya kupata kipaimara.
Mwandishi wetu aliwashuhudia wawili hao wakionekana dhahiri kuweka tofauti zao pembeni na kujali shughuli ya binti yao iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa mama mzazi wa Monalisa, Suzan Lewis ‘Natasha’, Yombo –Buza, Dar. 
Muda wote walionekana wenye furaha na waliketi kwenye meza moja huku Monalisa akionesha heshima wakati wa kumlisha keki Tyson kwa kupiga magoti.  
“Hawa jamani wanapendezana sana wakiwa pamoja. Jamani... mtoto wao amerudisha penzi lao. Ingefaa wakafikiria upya na kuona kuna umuhimu wa kurudiana na kumlea pamoja mtoto wao,” mmoja wa wageni waalikwa alisikika akisema. 
Katika kuonesha kuwa kweli hawana bifu, Mona aliamua kumtunza mzazi mwenzake noti nyingi za elfu kumikumi zilizokadiriwa kuwa zaidi ya 200,000 ambapo alisema: “Huwa nawashangaa watu wengi wakiwatuza akina mama kwa kuwalea vyema watoto lakini wanawasahau akina baba.
Sasa mimi namzawadia baba Sonia kwa sababu bila yeye, mtoto wetu asingekuwepo.”
Tukio hilo lilivuta hisia za watu na kusababisha shangwe kubwa kuibuka katika sherehe hiyo. 

MOJA KATI YA ALBAM ZA MUASISI NA MTENDAJI WA PATAPICHA

MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA BOB JUNIOR,MTOTO WAKE PAMOJA NA PETER NDANI YA STUDIO ZA DTV 
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA DAZ BABA NDANI YA KIPINDI CHA AREA 4 @ DTV
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA JERRY WA RHYMES NDANI YA STUDIO ZA DTV 
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA WADOGO ZAKE, KUTOKA KUSHOTO NI KIGUSA NGINILLA, DOCTOR KWANDU NA BERNADETHA (KUPIWA)
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA MENINA NDANI YA STUDIO ZA DTV
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA PENNY PLATNIUMZ 
MALIKA J, NGINILLA NA ROSE "ROZZAY"
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA MENEJA WA MAPACHA WATATU DACOTA DELAVIDA
MALIKA J, NGINILLA CHUONI BAADA YA KUTUNUKIWA DEGREE YAKE YA KWANZA
MALIKA J, NGINILLA CHUONI BAADA YA KUTUNUKIWA DEGREE YAKE YA KWANZA 
MALIKA J, NGINILLA PEMBENI JAPHET KASEBA 
MALIKA J, NGINILLA KISERIKALI ZAIDI AKIWA NA MKUU WA WILAYA YA MOROGORO MJINI, SAID AMANZI 
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA MUIMBAJI WANYIMBO ZA INJILI EDSON MWASABWITE PAMOJA NA MPIGAPICHA EMMANUEL EDWARD
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA RAFIKI YAKE MKUBWA SHAABAN MAPUNDA PAMOJA NA LECTURER, DOCTOR WAO NASSOR ALI
FAMILIA YA NGINILLA ENZI HIZO MALIKA YUKO MDOGO 
 
MALIKA J, NGINILLA AKIWA NA SHILOLE BAIBY NDANI YA KIPINDI CHA AREA 4 ON DTV

WATU WA-HACK ACCOUNT YA INSTAGRAM YA JOKETI MWEGELO "KIDOTI"


Ikiwa ni wiki kadhaa tangu Jacklyn Wolper kudhalilishwa kwenye ukurasa wa facebook,sasa leo yameibuka mengine kwa Jokate Mwegelo.
Jokate Mwegelo akionyesha kusikitishwa na kuwapa pole mashabiki wake kwa kile kinachoendelea instagram,baada ya watu kuibuka na kutumia jina lake vibaya katika mtandao huo,kisha kuwatapeli fedha mashabiki wake chini ya shilingi laki tatu.

JUMBA LA MSHINDI WA TUZO NYINGI ZA AMERICAN MUSIC AWARDS, TAYLOR SWIFT

Tuesday 26 November 2013

TIMBALAKE NA TAYLOR SWIFT WATAMBA TUZO ZA AMERICAN MUSIC AWARDS 2013


Mwanamuziki Justine Timberlake pamoja na Mwanamuziki Taylor Swift ndio wasanii walio ongoza kwa kupata Tuzo nyingi katika utoaji wa Tuzo za American Music Awards 2013 ambapo kila mmoja amejinyakulia tuzo 3.
Wasanii wengine Imagine Dragon waliofanikiwa kuchukua Tuzo ni kama ifuatavyo:

 Male Pop Rock Artist - Justin Timberlake
Favorite Female Artist, Soul/R&B - Rihanna
Favorite Album, Country - Red, by Taylor Swift
Favorite Album, Rap/Hip-Hop - The Heist, by Macklemore & Ryan Lewis
Favorite Artist, Alternative Rock - Imagine Dragons
Favorite Artist, Latin - Marc Anthony
Favorite Album, Pop or Rock - Take Me Home, by One Direction
New Artist of the Year - Ariana Grande

Favorite Male Artist, Soul/R&B - Justin Timberlake
Favorite Female Artist, Country - Taylor Swift
Single of the Year - “Cruise,” by Florida Georgia Line, featuring Nelly
Favorite Album, Soul/R&B - The 20/20 Experience, by Justin Timberlake
Favorite Artist, Electronic Dance Music (EDM) - Avicii
Favorite Male Artist, Country - Luke Bryan
Favorite Band, Duo or Group, Pop or Rock - One Direction
 
Artist of the Year - Taylor Swift