Sunday 14 July 2013

WATAZAMAJI WA MCHEZO WA STARS DHIDI YA UGANDA WADATA KWA HASHEEM THABEET

Watazamaji waliohudhuria kushuhudia mchezo kati ya Tanzania na Uganda wamejikuta wakipiga mayowe kama wamedata kumshangilia mtanzania anayecheza kikapu Nchini Marekani Hasheem Thabeet katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hasheem aliingia katika mchezo huo na kushangiliwa na mashabiki lukuki waliokuwa wamejaa uwanjani hapo na walionesha kumshangilia kwa kupiga mayowe kama ishara ya kumkukubali na kumpenda.
Baada ya kuingia uwanjani hapo alipita katika baadhi ya majukwaa na kuanza kusalimiana na mashabiki waliohudhuria kushuhudia kipute hicho.
HASHEEM THABEET AKIINGIA UWANJANI KABLA YA MCHEZO HUO
HASHEEM AKIPEANA MIKONO NA WASHABIKI WALIOPO MAJUKWAANI MARA BAADA YA KUINGIA USWANJANI HAPO
HASHEEM AKIWAPUNGIA MIKONO WATAZAMAJI KLABLA HAJAENDA KUKAA KWENYE KITI CHAKE
Hasheem yupo Nchini Tanzania kwa mapumnziko mara baada ya ligi ya kikapu ya NBA ya nchini Marekani kumalizika.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako