Ilikuwa Juni 18, mwaka huu katika Uwanja wa Soweto wanachama na wapenzi wa CHADEMA walikukusanyika ili kuwaaga watu wanne waliokufa kufuatia bomu lililolipuka Juni 15, katika uwanja huo.
Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini humo alifika uwanjani hapo kumwokoa baba yake Godwin Malisa ambaye ni mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha mbwa mwizi....Anaendelea kusema: “Nilimwambia baba tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa... ..Askari mmoja akasema ‘laleni chini’, tukalala tukidhani tutakuwa salama. Lakini walikuja askari na kutupiga marungu mwili mzima mimi na baba,... ” Mara wakatokea askari wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga mpaka mkono na mguu ya kushoto ikavunjika.
“Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba wakati askari wanatupiga. Askari mmoja alirarua gauni langu chini na juu, hadi nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya mapaja yangu ili alipue sehemu za siri, wenzake wakamkataza. Mwingine alisema kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia akasema watuue wote, mimi niliomba wasituue maana nimeacha mtoto mchanga nyumbani.”
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama wa Chadema.
“Walisema ‘unajifanya wewe Chadema, sasa ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea CCM wewe.’ Mimi niliwaambia sina chama chochote nimekuja kumwokoa baba yangu. Wakati huo wote walishanivua hereni, simu wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.”
“Kisha likaja gari la polisi tukabebwa na kuingizwa humo. Mwendo tuliondoka pale ulikuwa wa kasi huku wakiendelea kulipua mabomu na kutukanyaga bila kujali. Tulishtukia tuko Hospitali ya Mount Meru, tukabwagwa hapo na gari hilo likaondoka.”
Chanzo: Mwananchi - Juni 24 2013

No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako