Wednesday 17 July 2013

ALICHOWASISITIZA DE GEA KWA WAPENZI WA MANCHESTER UNITED

MLINDA mlango wa timu ya Mashetani wekundu wa Manchester United David De Gea amewataka mashabiki wa Manchester United kumfananisha yeye na magolikipa wazamani waliopata mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo akiwemo Edwin Van der Sar na Peter  Shemichel.
ALIYEWAHI KUWA GOLIKIPA NGULI WA MANCHESTER UNITED MDENISH PETER SCHEMICHEL
“Ni dhahiri kuwa nimebadilika sana ukinilinganisha na kiwango cha misimu iliyopita na hii inasababishwa na makocha mbalimbali wanaonielekeza ninapofanya mazoezi “ Alisema De Gea
 EDWIN VAN DER SAR
Alisema  najua nilitoka katika ligi tofauti na ya England na pia nilikuwa bado mdogo majukumu ya kukuwa kimazoezi yalikuwa yakinikabili na sikutegemea kukutana na nilivyovikuta huku lakini nafahamu nilitakiwa kuwa golikipa mwenye kiwango cha juu zaidi unaweza kuona sasa jinsi nilivyokuwa na misuli mikubwa nimekuwa nikifanya mazoezi magumu ya kunyanyua vitu vizito ni kweli ulikuwa ni ukatili mkubwa kwa mwili wangu” Alisema golikipa huyo
DAVID DE GEA ANAYEPENDA KUFANANISHWA NA NGULI WALIOPITA WA MANCHESTER UNITED
“ Nimekuwa nikibadilisha hata mlo wangu kwa kuacha kula vyakula vilaini na kula vyakula vitakavyonisaidia katika kujenga mwili kutokana na mazoezi ninayoyafanya
 Akiongelea Changamoto alizozipata katika klabu hhiyo ikiwemo katika mchezo dhidi ya Tottenham ambao walitoka sare anasema najua kitendo cha kufanya makosa katika mechi tuliyotoka sare na Tottenham kiliniweka katika wakati mgumu na muda mwengine nimekuwa hata  nikiwekwa benchi lakini hilo nimeichukua kama changamoto na sasa najiona niko fiti.
DE GEA AKIFANYA MOJA YA MAZOEZI YAKE KUJIWEKA FITI KWA MIKIKI MIKIKI YA LIGI KUU YA UINGEREZA
De gea anasema siku alivyosikia Edwin Van der ser anataraji kustaafu na yeye ndio angepdewa nafasi ya kumrithi alifurahi sana na kufikiria kutaka kuwa golikipa mkubwa kwenye  mwa midomo ya wapenzi wa Manchester United ili wanapozungumzia umahiri wa Van der sar na Schemichel  wawe wanamzungumzia yeye sawa na magolikipa hao kwa umahiri.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako