Wednesday 24 July 2013

BUYERN MUNICH YAIBAMIZA BARCELONA GOLI 2 - 0



Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, leo hii ameifunga timu hiyo ambao ndio mabingwa wa La Liga kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika huko Munich.

Philipp Lahm ndie aliyeanza kuingiza mpira nyavuni katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 14,  na Mario Mandzukic akaipatia Bayern bao la pili dakika ya 87.
Barcelona ilikuwa ikiongozwa na Jordi Roura, wakiwa bado wanamsubiri kocha wao mpya Gerardo Martino, walishindwa kutoka na ushindi katika mchezo huo, huku Messi akibadilishwa na Dongou.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako