Thursday 30 January 2014

AJALI YAKUTISHA MTU MMOJA AGONGWA NA TRENI NA KUKATIKA SEHEMU MBILI

Hii ni moja kati ya Ajali za kutisha sana kuwahi kutokea tangia kuanzishwa kwa usafiri wa treni katika jiji laa Dar es Salaam
Ajali hii imetokea Maeneo ya Mabibo mwisho wa lami mara baada ya mtu mmoja jina halikuweza kupatikana kwa haraka kutaka kuvuka upande wa pili kumbe ndio safari yake ya mwisho ilikuwa imewadia
Picha zinazofuata ni za kusikitisha sana na tunaomba radhi kwa picha hizi japo jamii inapasa kufaham.




Wednesday 29 January 2014

NYOKA WATUMIKA KUFANYA MASSAGE NCHII INDONESIA


Jinsi siku zinavyokwenda na mambo ndiyo yanazidi kubadilika.
Huko Jakarta, Indonesia katika sehemu ya Bali Heritage Reflexology wameanzisha massage mpya ambayo hutumia Nyoka mbalimbali kumfanyia massage mteja.
Kama Inavyoonekana kwenye picha kijana wa kiume akiwa ametulia akifanyiwa massage na Nyoka zaidi ya watatu.
Gharama ya kufanyiwa Massage kwa kutumia nyoka hao ni Paundi 30 ambazo ni sawa na Sh.66,000/= za kitanzania.
 

MSANII WA NIGERIA KCEE, AMLIPA NICK MINAJ MIL. ZAIDI YA 650 KUFANYA NAYE WIMBO


Habari kutoka kwenye mtandao moja wa burudani wa Nigeria zinadai kuwa msanii, KCEE ametoa kitita cha sh. zaidi ya milioni 650 kufanya wimbo na msanii wa kimataifa Nick Minaj.
"Tupo nchini Marekani kujaribu kupata Collaboration, Ni kweli tupo kwenye mchakato wa kufanya wimbo na Nick Minaj. Tulitaka kuifanya iwe ni Suprise kwa mashabiki lakini kwa kuwa tayari imejulikana hatuna budi kusema ukweli huo" Alisema 
Wakati mambo yakitaarifiwa hivyo, Meneja wa msanii huyo aligoma kutaja kiasi cha pesa walizompa Nick Minaj, "Kweli tumempa pase Nick Minaj ili tufanye naye Ngoa ila kiasi ni Siri yake, na kwa taarifa tu tunataka kuongeza msanii mwingine kutoka YMCMB ambaye ni zaidi ya Nick Minaj, Nick Mwenyewe ameshadhibitisha kufanya wimbo na KCEE ila huyo mwingine mtamjua tu" 

TECHNOLOGY INAVYOENDELEA KUKUA


DIAMOND AZIDI KUMNOGESHA WEMA SEPETU


Baada ya kupiga shoo ya nguvu Nchini Kenya, msanii anayeongoza kwa gharama za malipo ya shoo zake, Naseeb Abdul a.k.a Diamond aingia dukani na kumnunulia zawadi mpenzi wake.
Diamond alionekana akifanya manunuzi ya manukato mbalimbali Nchini Kenya ambapo muda mfupi baada ya kutua Dar, Mpenzi wake Wema Sepetu alipost Twitter akielezea Zawadi alizonunuliwa na Msanii huyo.

BABA YAKE NEYMAR AIPIGIA CHAPUO BARCA KUMSAJILI MWANAE

Baba wa mwanasoka Neymar ametetea suala la malipo ya kabla ya Paund million 10 ambayo Barcelona iliilipa kampuni yake miaka mitatu iliyopita ili kupata upendeleo katika kugombea saini ya mchezaji huyo.
Barcelona waliizidi nguvu Real Madrid katika kuwania saini ya mshambuliaji huyo, mwenye miaka 21 ambaye wiki iliyopita uhamisho wake ulileta matatizo Nou camp, na kumfanya Sandro Rosell kujiuzulu kuwa Raisi wa klabu hiyo baada ya kufunguliwa kwa kesi ya matumizi mabaya ya fedha katika usajili wa Neymar
Jana Jumanne, Neymar Jr alikiri Barca walimpa €10m mwaka 2011. Hii ilikuwa ni sehemu ya malipo ya €40m waliyomlipa kwa ujumla kuhakikisha Barca wanapewa nafasi ya kwanza katika uhamisho wowote wa Neymar, lakini akasisitiza kwamba hawakuvunja sheria kwa makubaliano hayo binafsi na ya siri. Fedha hizo ilizolipwa kampuni ya baba yake Neymar zingerudishwa endapo mchezaji huyo asingejiunga na klabu hiyo, alisema baba mzazi wa Neymar.  
“Barcelona walinilipa €10m [mnamo 2011],” Neymar Jr aliiambia ESPN Brasil, baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari nchini Brazil.
“Sio kosa la kisheria, Barca hawakumlipa Neymar, waliilipa kampuni yangu (N&N, inamilikiwa na wazazi wa Neymar].
“Nini nilifanyia zile €10m? niliziweka kwenye bima ili ikitokea chochote kwa Neymar, ikiwa angepata majeruhi, kwa mfano, bass ningeweza kulipa deni la €40m.”

SNAA LEE ARUDI STUDIO

Mwanamuziki wa Muda mrefu aliyetamba kwenye game la muziki anayejulikana kwa jina la Snaa Lee akiwa Studio za Baucha Record Kuandaa Track yake Mpya

RAIS WA BARCA ATAKA MESSI AONGEZEWE MSHAHARA, AMZIDI RONALDO


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hauzwi na klabu hiyo inapanga kujadili mkataba mpya na raia huyo wa Argentina, amesema rais wa klabu hiyo Joseph Maria Bartomeu.
Kuna uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne wa tuzo la Ballo d’Or, mwenye umri wa miaka 26, anatakiwa na matajiri wa klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain.
Katika mahojiano na kituo cha radio cha RAC1, yaliyonukuliwa katika mtandao wa Barcelona, Bartomeu anasema: “Klabu itakaa na kuangalia mkataba mpya. Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha kuwa yeye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara bora zaidi duniani.”
Messi alipachika wavuni mabao 60 katika mechi 50 aliyocheza msimu uliopita na hadi sasa amefunga mabao 18 na manane kati ya hayo ndiyo aliyoyafunga katika Ligi.

RONADINHO GAUCHO AHAMIA KWENYE MUZIKI

Mara nyingi inazoeleka kwa Star yoyote duniani kufanya kitu kilichosababisha awe star, yaani kama muimbaji atajitahidi kukomaa na uimbaji, kama ni mchezaji mpira atajitahidi kukomaa na mpira, japo kwa sasa tunawashuhudia wasanii wengi wa movie kwa Tanzania wakijaribu muziki na baadhi yao kupokelewa vizuri.
Miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliopokelewa vizuri wakitokea kiwanda cha Movie Tanzania kuna Shilole, Snura, Kitale, Baby Madaha, Marehemu Sharo Milionea na wengine wengi.
Kwa hapa nataka tumzungumzie Mwanasoka maarufu kutoka Brazil Ronadinho Gaucho ambaye ameonekana ana vipaji vingi mara baada ya kuonekana kwa video hii akiimba, nyimbo hii inahusu wale waliokata tamaa ya maisha.

JUX NAYE AVUTA MKOKO MPYA