Tuesday 23 July 2013

SAKATA LA UHAMISHO WA BALE NA TOTTENHAM LAFIKIA PATAMU

GAZETI la michezo la Marca la spain limeripoti winga wa timu ya Taifa ya Wales Gareth bale amekubali kujiunga na Real Madrid kwa dau litakalomlipa euro milioni 8.5 kwa mwaka.
KOCHA WA TOTTENHAM HOTSPURS VILAS BOAS
Gazeti hilo limeripoti kuwa Bale tayari ameiambia Tottenham anataka kuondoka kwenda Bernabeu na hivyo anataka ruhusa ili aweze kwenda kusaka maisha sehemu nyingine.
GARETH BALE NA MIONGONI MWA TUZO ZAKE ALIZOCHUKUA NA LIGIM KUU YA UINGEREZA
Pamoja na Bale kutoa ombil hilo, kocha wake Vilas Boas akiongea na vyombo vya habari nchini Hong kong amesema itakuwa ni vigumu kumuuza bale kwani kufanya hivyo kutawafanya wapunguze uwezo wao kushindania nafasi za kucheza klabu bingwa ulaya na kombe la ligi kuu ya Uingereza.

Akitoa ufafanuzi ligi iliyopita Boas alisema msimu huo ulimalizika na wao kukosa nafasi ya kucheza kombe la mabingwa ulaya hivyo wanataka kuhakikisha wanaongeza juhudi kufikia malengo yao, na wanaweza kufanya hivyo wakiwa na bale.

Kocha huyo alisema Bale ni mchezaji mwenye hadhi ya Dunia narudia kusema maneno niliyoyatoa msimu uliopita ya kuwa tunataka kushinda vikombe tukiwa naye hivyo sitakuwa tayari kumuona akiondoka klabuni kwetu na kutimkia kwengineko
LOVE U ALL

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako