Wednesday 31 July 2013

GARI ILIYOBEBA NYANYA YAPATA AJALI MINDU

GARI aina ya ya lsuzu lenye namba za usajiri T749 CCG iliyokuwa akisafirisha matenga ya nyanya kutoka Kijiji cha Mlali kuelekea kwenye moja ya masoko ya mji wa Morogoro jana mchana limepindua eneo la Mindu jirani na bwawa la Mindu.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba gari hilo lilipinduka baada ya kujaribu kumkwepa dereva wa boda boda na kwamba katika ajari hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya wamiliki wa mizigo hiyo walijerehiwa.

'Unajua hivi vigari ni vyepesi sana hivyo kikiyumba kidogo  kina pinduka, wafanyabisha kwa kawaida huwa wanakaa jua ya matenga yao lakini kwenye tukio hili wamilikiwa matenga hayo ya nyanya walikaa kwa dereva, sipati picha kama wangekaa juu ya matenga yao kama wanavyokaaga siku zote"alisema shuhuda huyo aliyejitambulishwa kwa jina la Johnson Joseph. 


Source: Shekidele blog 

BONDIA MTANZANIA AMCHAKAZA MTHAILAND.

BONDIA OMARI KLIMWERI AKITANGAZWA KUWA MSHINDI KATIKA PAMBANO HILO

BONDIA Omar Kimweri anayefanya shughuli zake nchini Australia amemchakaza Bondia wa Thailand anayejulikana kwa jina la Ekkalak Saenchan katika raundi ya kwanza.
BONDIA OMARI KIMWERI AKIMTUPIA KOMBORA BONDIA WA KITHAILAND

BONDIA OMARI KIMWERI AKIMTUPIA KOMBORA BONDIA WA KITHAILAND

KIMWERI AKIMVIZIA MTHAILAND AMPE MAKONDE MAZITO
Huku kukiwa na wimbi la mabondia wa kitanzania wanaopighwa ovyo wanapojaribu kupambana mapambano nje ya nchi na kufanya m,abondia wa kibongo kuonekana mdebwedo lakini haikuwa hivyo kwa mtanzania huyo.

PATAPICHA INAMPONGEZA KWA KUWATOA WATANZANIA KIMASOMASO NA KUWATAKA WENGINE WAONGEZE JITIHADA
source superd blog

KITU CHA MWISHO WANACHOJIANDAA KUKIFANYA MAN UNITED KUMSAJILI FABREGAS

MANCHESTER UNITED WATAWEZA KUSAJIL;I KIUNGO HUYO AMBAYE KOCHA WA BARCA BADO ANATAKA KUENDELDEA KUFANYA NAE KJAZI NDANI YA TIMU HIYO.

MANCHESTER UNITED wanajiandaa kuvunja rekodi ya usajili kwa klabu yao kumsajili Cesc Fabregas kutoka klabu ya FC BARCELONA.Habari kutoka katika gazeti la Daily Mail la Uingereza linasema kuwa Mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza watatoa dau la paundi million 35 kama ofa ya mwisho kumnasa kiungo huyo.

KOCHA WA MAN UNITED ANAYEMMEZEA MATE KIUNGO FABREGAS WA BARCELONA

Tayari Manchester wameshatuma dau la paundi millioni 26 na 30 kabla ya kukataliwa na mabingwa hao wa Hispania. Ingawa Barcelona wametangaza waziwazi kutomuuza Fabregas, haswa kutokana na kocha mpya wa timu hiyo aliyesema anataka kufanya kazi na Fabregas na hivyo hayuko tayari kuona anauzwa.

FABREGAS

REKODI YA UNUNUZI WA WACHEZAJI KWA KLABU YA MAN UNITED
  • Roy Keane kutoka Nottingham Forest, Paund 3.75m (July 1993)
  • Andy Cole kutoka Newcastle, Paund 7m (January 1995)
  • Jaap Stam kutoka PSV, Paund 10.75m (July 1998)
  • Dwight Yorke kutoka Aston Villa, Paund 12.6m (August 1998)
  • Ruud Van Nistelrooy kutoka PSV, Paund 19m (July 2001)
  • Juan Sebastian Veron kutoka Lazio, Paund 28.1m (July 2001)

KAVUMBAGU AJIGAMBA KUWA KINARA WA USHINDANI WA NAMBA YANGA

KAVUMBAGU AKITAMBULISHWA SIKU YAKE ALIPOSAJILIWA NA YANGA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Didier Kavumbagu, raia wa Burundi, amekiri kuwa kutakuwepo na ushindani wa namba msimu ujao wa l;igi katika timu hiyo lakini akasema anajipanga kuhakikisha anakabiliana na hilo.
Didier Kavumbangu mchezaji wa Yanga aliyesajiliwa toka timu ya Olympique kutoka Burundi akionekana haswa kutoka katika michuano ya kombe la Kagame, Amesema atahakikisha anajifua kwa bidii zaidi ali awe fiti na aweze kumshawishi kocha wa Yanga Brants aweze kumpanga katika kikosi hicho cha mabingwa wa soka wa Ligi kuu ya Tanzania bara

“Ninakubali na najua kuwa kutakuwa na ushindani mkubwa t “Nitajituma kwa nguvu zangu zote kuhakikisha sipotezi nafasi yangu,” alisema Kavumbagu.faut naule wa msimu uliopita lakini najitahidi kuhakikisha sipotezi nafasi yangu Alisema Kavumbagu.
KAVUMBAGUUUUUUUU
Alisema najuakusajiliwa kwa washambuliaji wengi kwenye timu yetu kumefanya kuwa na changamoto na nitakuwa nashindania namba dhidi yao lakini najianmini na naamini nitashinda katika hilo kwa maendeleo ya timu yangu.

MBEYA BABA AMBAKA MWANAWE NA KUMZALISHA


YUSSUF AMANI ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA DAMU

MAHAKAMA ya mkoani Mbeya imehukumu kifungo cha kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Bw Yusuf Aman baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 15( jina linahifadhiwa).
NI AIBU SANA BWANA AMANI AKIJIZIBA SURA KUKWEPA CAMERA ZA WAANDISHI WA HABARI KUPATA SURA YAKE
Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo BwYusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
  
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.
  
akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.

Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.

Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.

Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
KULIA NI MTOTO ALIYEZALISHWA NA BABAAKE AKIWA AMEBEBA MWANAWE HUYO
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa  Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.

Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.

Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.

Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa” Na kasha kutoa hukumu hiyo

PATA PICHA INALAANI KITENDO HICHO NA KUTOA POLE KWA WALE WOTE WALIOPATWA  NA MKASA HUO.