Wednesday 15 April 2015

MECHI ZA UEFA HATUA YA MTOANO ROBO FAINALI-------------

Katika Jiji la Madrid huko uhispania kulikuwa hapatoshi katika mchezo uliowakutanisha Miamba ya jiji hilo, Atletico Madrid na Real Madrid ambazo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya, hatua ya robo fainali.
Atletico waliowakaribisha Real katika mchezo uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon, ambapo timu hizo zitarudiana katika uwanja wa Santiago Bernabeu tarehe 22 Aprili.
mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak alikuwa kikwazo kwa real, ambaye alinga'ara katika mchezo huo kwa kupangua michomo mikali kadhaa ya wachezaji wa Real Madrid walokuwa wakilisakama lango la atletico, huku Mario Suarez wa Atletico Madrid akikosa nafasi ya kuifungia timu yake mwishoni mwa mchezo huo.
Naye winga Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale aliyekosa nafasi muhimu mapema katika dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza cha mchezo kwa kushindwa kutumbukiza mpira wavuni amesema walistahili kushinda, ingawa haikuwa hivyo.
 “NI MATOKEO MAZURI KUENDEA HATUA YA MARUDIANO KWA SABABU HATUKURUHUSU GOLI LOLOTE. KWA UPANDE WANGU NAFKIRI TULITAKIWA TUSHINDE, TULISTAHILI KUSHINDA KWA SABABU KIPINDI CHA KWANZA TULICHEZA VIZURI ZAIDI YA ATLETICO BAHATI MBAYA HATUKUWEZA KUENDELEZA KIWANGO KILE KILE KIPINDI CHA PILI”.
Katika mchezo huo Mlinda mlango wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas ameweka historia yake kwa kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi katika michuano hiyo kwa kufikisha michezo 147 akimzidi mchezaji wa Barcelona xavi Hernandez.
Mechi hii jana pia imeweka rekodi kwa Vijana wa Carlo Ancelotti kuwa ni mchezo wao wa saba kukutana na Atletico Madrid bila kushinda.
Mchezo mwingine uliochezwa jana usiku ulizikutanisha timu Juventus ya Italia na Monaco ya Ufaransa, Matokeo ya mchezo huo Juventus iliibuka na ushindi wa goli 1-0. Juventus ilipata bao lake pekee katika dakika ya 57 kwa njia ya penalti ikifungwa na Arturo Vidal.
Hata hivyo kocha wa Monaco Leonardo Jardim, ameilalamikia penalti hiyo kuwa haikuwa ya haki. Timu hizi nazo zitarudiana huko Monaco April 22.
Juventus inalenga pia kufika hatua ya nusu fainali ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.
Wakati huo huo, winger wa monaco Nabil Dirar anaamini mshambuliaji wa timu hiyo aliye kwa mkopo katika timu ya man utd Radamel Falcao atafkiria kurudi Monaco na anatamani asingeondoka Monaco.
Falcao alitimkia man utd kwa mkopo wa muda mrefu lakini amekuwa katika wakati mgumu chini ya van gaal ambaye amekuwa akimuweka benchi.
Mshambuliaji huyo raia wa Colombia amefunga goli nne tu kwa man utd hali inayopelekea utd kusita kulipa kiasi cha pauni milioni 53 ili kumsajili kwa ujumla.
Michezo mingine miwili ngazi ya robo fainali itaendelea leo usiku ikizikutanisha timu ya FC Porto ya Ureno dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, huku Paris Saint Germain ya Ufaransa ikiikaribisha Barcelona ya Hispania.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa aina kutokana na kila timu kuonekana kuwa tishio kwa wapinzani wao.
Timu ya PSG itakosa huduma ya mshambuliaji wake hatari Zlatan Ibrahimovic ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa dhidi ya mechi na Chelsea pamoja na Aurier, kwa upande wa majeruhi watakosa huduma ya Thiago motta pamoja na mlinzi wao david luiz aliye na hati hati ya kucheza.
Kwa upande wa barca wataikosa huduma ya Dani alves pamoja na Thomas vermaelen.
Hata hivyo kocha wa PSG Laurent Blanc amesema hadhani kama falsafa za Barcelona zimebadilika sana na kuongeza kuwa ni kweli wanamiliki mpira vizuri na wana nguvu ingawa na wao wanapenda kumiliki mpira.
Blanc amesema wanaweza kuwafunga barca kwani wao ni moja ya timu chache zilizowahi kuwafunga Barca goli 3.