Wagosi wa
kaya wameendelea kutuma salamu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara
kwa kuwachapa 1-0 Simba SC kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya wa
ligi kuu ya Vodacom.
KIKOSI CHA COASTAL UNION KIKIPASHA MISULI MOTO KABLA YA MCHEZO |
Mfungaji wa bao
hilo ni mshambuliaji Mkenya, Crispian Odula aliyesajiliwa kutoka Bandari ya
Mombasa.
Mechi hiyo
iliyohudhuriwa na mashabiki wengi uwanja wa Mkwakwani, ilikuwa gumzo kwenye
viunga vya mji wa Tanga na Dar es Salaam ambapo Simba waliingia jijini hapo
wakijitapa kulipiza kisasi cha msimu uliopita baada ya kubaniwa kupata point za
bure na kutoka suluhu.
Kipindi cha
kwanza timu zote zilicheza kwa kujihami huku kukiwa na mashambulizi ya
kushtukiza ambapo mpaka dakika 45 za mwanzo hakuna timu iliyoona lango la
mwenzake.
Kipindi cha
pili Coastal Union waliingia kwa kasi na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara
kitu kilichompa wakati mgumu golikipa wa Simba, Mganda Abel Dhaira.
Kufikia
dakika ya 54 Crispian Odula anayeheshimika sana ndani ya jiji hilo alipokea
pasi safi kutoka kwa Keneth Masumbuko, akauacha udunde ndani ya eneo la hatari,
akaja mchezaji wa Simba akampiga tobo akainua macho kumuangalia Mganda Dhaira
akamekaa uelekeo gani, alipoona amekaa katikati ya lango akapiga kwenye nyavu
ndogo na kuwatia wazimu mashabiki wa Coastal Union waliojaa ndani ya uwanjani utadhani
hakuna Ramadhani.
Kitu
kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu ni kuona kama mchezaji chipukizi aliyetoka
Coastal Union, Ibrahim Twaha ‘Messi’ atacheza ama la, lakini kufika dakika ya
70 aliingizwa kuongeza mashambulizi baada ya Simba kuelemewa. lakini kocha
Morocco alifanya ujanja kwa kumuingiza kijana mwenzie waliocheza pamoja timu B,
Hamad Juma ‘Basmat’.
WACHEZAJI WA TIMU ZOTE MBILI SWAKIKAGULIWA KABLA YA MCHEO KUANZA |
Kazi ya
‘Messi’ ikawa imeishia hapo kwani Hamad alipewa kazi moja tu ya kuhakikisha
‘Messi’ akifika winga ya kushoto ilipo ngome yake hapigi krosi.
Mbwana
Kibacha na Juma Nyosso wakaambiwa wahakikishe kijana huyo mwenye mbio nyingi
havuki ukuta wa Coastal Union. Mwisho akaonekana hana msaada wowote kwa timu
namna alivyodhibitiwa.
Kikosi cha
Coastal Union: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha, Othman Bakari, Juma Said ‘Nyosso’,
Marcus Ndehele, Jerry Santo, Uhuru Suleiman, Crispian Odula, Keneth Masumbuko, Haruna
Moshi ‘Boban’, na Daniel Lyanga.
WACHEZAJI WA COASTAL UNION WAKISHANGILIA BAO LAO LILILOFUNGWA NA CRISPIAN ODULA KIUNGO TOKA KENYA |
Baadaye
kocha mkuu wa coastal Union akishirikiana na Ally Kidi walifanya mabadiliko
kwenye kipindi cha pili kwa kuwatoa
Uhuru Suleiman, Daniel Lyanga, Crispian Odula na Othman Bakar . Wakaingia Abdi
Banda, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Mohammed Sudi na Hamad Juma ‘Basmat’.
HABARI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA COASTAL UNION
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako