Saturday 20 July 2013

STEFAN JOVETIC AKITAMBULISHWA NDANI YA UWANJA WA MANCHESTER CITY


MANCHESTER CITY wamethibitisha kumsajili Mchezaji Stefan Jovetic kutoka klabu ya Fiorentina  kwa dau la paundi million 25.8 baada ya mshambuliaji huyo raia wa Montenegro kufaulu vipimo vya afya.
JOVETIC AKIWA NA JEZI ATAKAYOITUMIA MANCHESTER CITY

Inaeleweka kuwa Manchester City watatakiwa kulipa paundi millioni 22.4 kama dau la awali na kuongeza dau hilo kufikia paundi million 25.8 endapo mchezaji huyo atafanya vizuri.
JOVETIC AKIFANYA MAVITUZ YAKE UWANJANI
Anajiunga na timu ya Manchester  City na kukutana na mchezaji mwenzake aliyewahi kucheza nae Fiorenina, Matija Nastatic ambaye anacheza katika klabu ya matajiri hao wa jiji la Manchester.
JOVETIC AKIINGIA KATIKA UWANJA WA ETIHAD

Mchezaji huyo anataraji kujiunga na wenzake walioko katika ziara ya kujiandaa na msimu ujao  wikiendi hii.

Jovetic ameiwakilisha timu ya taifa ya Montenegro tangu mwaka 2007 akicheza mechi 27 na kufunga mabao 10.
NDANI YA POZI JOVETIC AKIPIGA PICHA KATIKA MAPOZI MBALIMBALI WAKATI AKITAMBULISHWA UWANJA WA MANCHESTER CITY ETIHAD

Jovetic anakuwa mchezaji wa nne kununuliwa katika majira haya ya kiangazi baada ya Fernadinho (paundi million 30),Jesus Navas(paundi million 15), Alvaro Negredo paundi million 20.6)  
FUNDI WA MAPOZI NA FOOTBALL PIA UNAMUONAAA KATIKA POZI MBALIMBALI
JOVETIC AKIWA KATIKA CHUMBA CHA KUVALIA NGUO CHA MANCHESTER CITY MARA BAADA YA KUTAMBULISHWA

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako