Monday, 22 July 2013

MAKAMBA AKOMA NA MESSEJI ZA WANANCHI KUHUSU KODI YA....!



“Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni ……..) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali.”aliandika Mnyika katika taarifa yake. 


Mambo yalikuwa tofauti baada simu yake kugeuka kuwa ‘public suggestions box’ iliyobeba kila aina ya jumbe za ajabu na matusi huku wengine wakidiriki kumpigia kitu ambacho kiligeuka kero kwake.

Makamba alitumia ukurasa wake wa facebook kuelezea kile kilichomkuta huku akilaani kitendo alichokifanya Mh John Mnyika.
  John Mnyika kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa. Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo.” Ni sehemu ya alichokiandika Makamba.

Hata hivyo pamoja na hayo yote anaamini kuwa hayo yataisha hivyo asibadili namba yake ya simu. 
My phone constantly engaged with nonstop calls and clogged with hundreds of messages. I hope this stops so I don't have to change my number. — January Makamba (@JMakamba)
Nae dada yake January Makamba ‘Mwamvita Makamba’ alionesha kuumizwa na kile alichokifanya Mnyika na kumtumia ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter akimtaka aombe radhi kwa kuwa yeye ni bora ya kile alichokifanya, na kwamba yeye ameziona jumbe zilizotumwa kwa kaka yake. 

John @jjmnyika I have seen the horrible SMS sent to January.What you did is unacceptable and deserves an apology. You are better than this — Mwamvita Makamba (@Makambas) Uamuzi wa bunge kupitisha tozo la kodi ya kadi za simu kwa mwezi kwa wananchi umepingwa vikali na wananchi lakini pia asilimia kubwa ya wabunge wanaoulizwa kuhusu uamuzi huo nao wanaonekana kupinga hoja hiyo na wengine wakirusha lawama zao kwa ‘serikali’…Japo ukweli unabaki palepale kuwa wabunge (asilimia kubwa) ndio waliopitisha mswada huo bungeni.

 January Makamba anakiri kuwa wabunge walishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini.
“Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini.” Aliandika Makamba katika sehemu ya ujumbe wake kupitia ukurasa wa facebook. 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako