Monday 15 July 2013

DIAMOND APIGIWA SIMU NA PREZZO KUOMBWA MSAMAHA


Msanii mwenye mafanikio na kipenzi cha wengi hapa nchini Nassibu Abdul almaaruf kama Diamond Plantinium leo ameujulisha umma ya kuwa msanii mwenzake waliyekuwa kwenye biff la kimaneno C.M.B Prezzo amemuomba msamaha kwa njia ya simu kufuatia tweet alizoandika hivi karibuni.
Diamond ameyasema hayo leo mchana wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Kenya kiitwacho Citizen kwenye kipindi cha Mambo mseto kinachoendeshwa na tangazaji William Tuva.
Diamond amezungumzia msamaha huo ya kwamba hauko na nia ya kweli kwani angetaka kumuomba msamaha asingempigia simu bali angeomba msamaha huo hadharani kwenye mtandao wa twitter kama alivyofanya kwenye diss zake.
Msanii huyo anayeongoza kwa kulipwa hela nyingi kwenye shoo zake (mwezi wa Sita na wa saba alijikusanyia zaidi ya Milioni 200) amesema alishangazwa na kitendo cha Prezzo kum-diss kutokana na majigambo aliyoyatoa kabla ya show yao kwenye Tamasha la Matumaini mwanzoni mwa mwezi huu, tamasha lililofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
“sikujisikia vizuri kabisa, vitu vingi vimezungumzwa kwanini anitukane, mimi sijazoea mambo hayo, tuachane na mambo ya kizamani ya kutengeneza attention kupitia ugomvi bali tutengeneze ngoma kali, haina haja ya kugombana” alisema Diamond
Rais huyo wa Wasafi ametoa ushauri kwa wasanii wote wa Afrika Mashariki kuwa wanatakiwa kuungana ili kuupeleka juu muziki wa kizazi kipya ili kwenda sawa na wanamuziki wa Afrika Magharibi.
“Sikupenda kama binadamu wa kawaida na sikujisikia vizuri East Africa hatuna muda wa kugombana, majigambo ya wasanii kuhusu kuzidiana fedha hayana maana yeyote istoshe hakuna mwanamuziki mmwenye hela East Afrika, tufanye kazi nzuri kuleta sifa kwenye nchi zetu”
Hata hivyo aliongeza ya kuwa licha ya kuumizwa na kitendo hicho hc aPrezzo hana tatizo naye.
Katika hatua nyingine Diamond ameeleza yupo mbioni kufanya ngoma na Jose Chameleone wa Uganda ambaye siku za karibuni alikuwa na Ziara nchini Marekani
                                      

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako