Mtanzania Sykes Omary enzi za uhai wake |
Polisi
nchini Marekani wameutambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa
kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku, wiki hii.
Wakielezea
kuhusiana na tukio hilo Afisa wa Polisi alisema Omar Sykes 22, na mwanafunzi
mwenzake walikuwa wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya
saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili na kuanza kuwashambulia kwa nia ya
kuwaibia.
Polisi
wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya
wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes, ambapo alifikwa na umauti alipofikishwa
kwenye hospitali ya maeneo ya jirani.
“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao
waliibiwa mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa
kituo cha polisi DC alipohojiwa na kituo cha News4.
Mwanafunzi
mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana
majeraha makubwa sana.
“Wanafunzi
wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha
sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka kituo cha News4.
Maelezo
kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya
kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu
kwa wahalifu hao kujulikana.
Sykes
alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa
Our Black Pages mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa
anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu
utafanyika shuleni kwao Jumamosi ya leo kuanzia saa 1 usiku.
Chuo kikuu
cha Howard kimetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Sykes:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea
nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea
na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili
kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote
walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha
itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote
watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.”
PATAPICHA
inawapa pole wazazi wa Sykes, ndugu jamaa na marafiki pamoja na watanzania wote
walioguswa na tukio hili
MUNGU AILAZE
MAHALI PEMA ROHO YA MAREHEMU SYKES
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako