Monday 15 July 2013

MWANAMITINDO KUTOKA TANZANIA APATA DILL YA MATANGAZO NA ADIDAS


Daniel David Mtanzania aliyezaliwa na kukulia kwenye mambo ya uanamitindo.
Jina lake anaitwa Danny David ni Mwanamitindo wa kiume toka Tanzania na mwanamitindo pekee toka Tanzania alipata nafasi ya kufanya kazi ya kutangaza nguo na viatu vya kampuni kubwa ya Adidas tawi la Afrika ya kusini.

Alianza kuonekana kwenye fashion mwaka 2012 kwenye maonesho ya Swahili Fashion Week chini ya mwanamitindo maarufu nchini Mustapha Hassanali, pia amewahi kushiriki kuonesha mavazi kwenye Harusi fashion week iliyofanyika chini ya mbunifu wa mavazi Ally Rehmutula bila kusahau alishawahi kushiriki na kushinda kwenye mashindano ya wanamitindo ya Maridadi model search yaliyofanyika hapa Tanzania.
Danny ni mwanasheria kitaaluma na ana degree ya sheria kutoka chuo cha Tumaini Iringa, katika interview aliyofanya na Magazine moja maarufu jijini Afrika Kusini hivi karibuni Danny amesema pamoja na kuwa mwanamitindo anamipango ya kuwa muigizaji kwani ni kitu alichokuwa anapenda kukifanya tangu utotoni
Hizi ni baadhi ya picha alizopiga akiwa nchi (picha zimepigwa na Ally Zoeb wa AZH Photography)

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako