Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili nchini Uganda jioni ya leo katika
uwanja wa ndege wa Entebe Kampala tayari kuikabili Uganda the Cranes kwa mechi
ya marudiano kutafuta tiketi ya kucheza katika mashindano ya CHAN.
Kikosi
hicho chenye wachezaji 20, kiliwasili muda mfupi baada ya saa kumi alasiri huku
wachezaji na benchi la ufundi wakiwa na matumaini makubwa.
Akiongea
mara baada ya kuwasili Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen alisema wamejiandaa
vizuri wakiwa Mwanza na ana imani kikosi chake kitabadili matokeo ya awali
ambapo Stars ilifungwa 1-0 na Cranes Jijini Dar es Salaam.
Alisema
licha ya kuwakosa wachezaji Shomari kapombe na Mwinyi Kazimoto, ana imani na
kikosi chake kuwa kitafanya makubwa Jijini Kampala.
“Tumekuja
kubadilisha mahesabu kwani tumejiandaa vizuri kabisa,” alisema Poulsen.
Mechi
hii ni gumzo kubwa Jijini Kampala kwani baadhi ya waganda wana hofu kuwa henda
wakafungwa nyumbani kwao.
Mechi
hii itapigwa katika Uwanja wa Namboole Jijini Kampala Jumamosi hii saa kumi
jioni.
Mashindano
ya CHAN yanatarajiwa kufanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Wachezaji na Benchi la Ufundi (Taifa Stars) wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda jioni ya leo tayari kuikabili Uganda The Cranes Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako