Monday 15 July 2013

WANACHOKIFANYA MANCHESTER BAADA YA KUMKOSA THIAGO ALCANTARA.

BAADA ya kushindwa kumsajili Thiago Alcantara na kushuhudia akisajiliwa na Bayern Munich, klabu ya Manchester United imegeuzia jicho lake kwa kiungo ces Fabregas kwa kutoa ofa ya dau la paundi million 26 kwa Barcelona iliwaweze kumsajili kiungo huyo.
Moyes anamuona Fabregas kama kiungo pekee aliyebaki mwenye ujuzi wa kuja kuisaidia safu ya ushambuliaji ya Manchester United kuendelea kuzitesa klabu nyengine barani ulaya.
Ingawa Mnchester wanaonekana kutulia kwanza katika mbio za kumfukuzia kiungo wa Real Madrid luka Modric lakini wanaonekana wako siriasi kutaka kumnasa Fabregas na watakuwa tayari kuongeza dau hilo mpaka kufikia paundi million 30 za uingereza.
FABREGAS ANAYEWANIWA NA MAN UNITED AKISHANGILIA MOJA YA MAGOLI YAKE NDANI YA KLABU YA BARCELONA
FABREGAS NA WIFE WAKE
FABREAGAS NA SWAIBA WAKE VAN PERSIE ... JE FABREGAS ATAMFUATA VAN PERSIE  ILI WARUDIE ENZI ZAO KATIKA KLABU MPYA YA MAN U NGOJA TUONE

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako