Saturday 20 July 2013

ARSENAL WANAVYOKARIBIA KUMSAJILI LUIS SUAREZ

Liverpool
MATUMAINI ya klabu ya Arsenal kumsajili Luis Suarez  yanaonekana kushika kasi baada ya Timu hiyo kusema kuwa iko tayari kufanya lolote kuhakikisha inamnasa mshambuliaji huyo aliyeonesha nia ya kutaka kukipiga katika klabu hiyo ya washika bunduki wa jiji la London.
Arsenal walituma ofa ya paundi millioni 30 kutaka kumnasa Luis Suarez lakini wakajibiwa na Liverpool kama wanataka kumnasa mshambuliaji huyo basi waongeze dau na kufikia Paund million 40
MCHEZAJI SUAREZ HUPENDA SANA KUOKOTA MIPIRA NDANI YA NYAVU MARA  BAADA YA KUZIFUMANIA NYAVU
Suarez ameonesha nia ya kutaka kujiunga na washika bunduki hao mara baada ya kuonesha kuvutiwa kutokana na ofa wanazotuma kutaka kumsajili  hivyo kuonekana kama vile Suarez amekiuka kauli yake mwenyewe ya kwamba hataondoka kuelekea klabu yoyote na kuiacha Liverpool.
KAMA UNALIKUMBUKA BIFU LA SUAREZ NA PATRIC E EVRA NDIPO HAPA LILIPOTOKEA
Inafahamika kuwa pamoja na Suarez kuonesha nia ya kutaka kujiunga na Arsenal lakini nia yake hiyo inaweza kukwama kutokana na sera ya Arsenal kutopenda kutumia pesa nyingi katika kusajili wanadinga haswa baada ya siku chache kushindwa kuafikiana na Real Madrid kumsajili mshambuliaji wa kiajentina Gonzalo 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako