Friday 19 July 2013

MABESTE APATA MTOTO WA KIUME

Msanii wa Kizazi kipya William anayejulikana kwa jina la MABESTE "Buuda" amefanikiwa kupata mtoto wa kiume mida ya saa 12 jioni katika Hospital ya Masana iliyopo Mbezi Beach.
Akizungumza na PATAPICHA Saa 2 usiku wa leo amesema anamshukuru mungu kwa kumpatia mtoto huyo wa kiume aliyempa jina la Kenrick William.
 Mabeste kwa furaha aliendelea kuelezea jinsi alivyopata taarifa ya kujifungua kwa Mpenzi wake amesema "leo tulikuwa tumefanya Shopping ya vitu kadhaa za mtoto kwa sababu kuna chumba nimetengeneza cha mtoto wife akaniambia kuna baadhi ya sehemu ya chumba waweke sticker za mtoto sasa wakati tunarudi mimi nikamuacha Mikocheni kwa dada yake nikaenda Sinza kuna mtu nilikuwa nakwenda kuongea naye biashara fulani, nikapigiwa simu na dada yake akiniambia hali ya mke wangu sio nzuri, So nikamwambia chukue usafiri ampeleke Hospital"
Akaongezea ya kuwa mke wake  akapelekwa Hospital mida ya saa 10 na kupewa kitanda baada ya masaa manne akafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume mwenye afya ya kutosha.
Mwandishi wa Story hii amefanya Mahojiano na Mabeste kwenye simu na hii ni sehemu ya Mahojiano hayo kwa ufupi.
 
Habari kamili pamoja na picha endelea kutembelea www.patapicha.blogspot.com pia tizama DTV 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako