Wednesday 31 July 2013

GARI ILIYOBEBA NYANYA YAPATA AJALI MINDU

GARI aina ya ya lsuzu lenye namba za usajiri T749 CCG iliyokuwa akisafirisha matenga ya nyanya kutoka Kijiji cha Mlali kuelekea kwenye moja ya masoko ya mji wa Morogoro jana mchana limepindua eneo la Mindu jirani na bwawa la Mindu.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba gari hilo lilipinduka baada ya kujaribu kumkwepa dereva wa boda boda na kwamba katika ajari hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya wamiliki wa mizigo hiyo walijerehiwa.

'Unajua hivi vigari ni vyepesi sana hivyo kikiyumba kidogo  kina pinduka, wafanyabisha kwa kawaida huwa wanakaa jua ya matenga yao lakini kwenye tukio hili wamilikiwa matenga hayo ya nyanya walikaa kwa dereva, sipati picha kama wangekaa juu ya matenga yao kama wanavyokaaga siku zote"alisema shuhuda huyo aliyejitambulishwa kwa jina la Johnson Joseph. 


Source: Shekidele blog 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako