Aliyekuwa
golikipa namba moja na nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja ametoa la moyoni
akisema atakuwa tayari kutaja timu atakayoichezea msimu ujao baada ya kutoka
Kampala nchini Uganda alikokwenda na timu ya taifa ya Tanzania
Kaseja
amesema tayari anajua anachokifanya na atakuwa wazi atakapocheza msimu ujao
baada ya kumaliza majukumu hayo ya timu ya taifa inayosaka tiketi ya kucheza
fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN dhidi ya Uganda The
Cranes, mchezo utakaochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa Nelson
Mandela.
Golikipa
huyo ambaye alikuwa chaguo la kwanza la makocha wote waliopita kwenye klabu ya
Simba na pia ndiye aliyekuwa nahodha wa klabu hiyo kabla ya mkataba wake
kumalizika na viongozi wa klabu hiyo wamesema hawatamuongeza mkataba.
Kaseja
amesema kuna timu nyingi zimejitokeza kuitaka saini yake ikiwemo vilabu vya
ndani na nje ya nchi lakini mara kadhaa imekuwa ngumu kukubaliana navyo
kwasababu viko chini ya dau analolitaka.
Hata
hivyo amesema pamoja na baadhi ya timu zilizojitokeza kuwa na dau dogo lakini
kuna timu nyingine zimefika dau lakini bado hajamalizana na timu yoyote
akiendelea kutafakari na atakaporejea kutoka Uganda atakuwa kwenye nafasi nzuri
ya kuweka wazi kila kitu.
Kaseja
amedumu kwenye klabu ya Simba kwa zaidi ya miaka 10 akijiunga kutokea Moro
United na alicheza kwa msimu mmoja katika timu ya Yanga.
Amesema
ameifanyia mengi makubwa klabu ya Simba na anaamini maamuzi hayo yaliyofikiwa
yanafungua milango mingine katika maisha yake huku akiwashukuru wale wote
wanaomtakia mema na wale wanaompiga mizengwe, yote akimuachia Mungu.
Ukiondoa
Moro United,Kaseja amechukua ubingwa wa ligi kuu akiwa na Simba na akiwa na
Yanga lakini ikumbukwe pia mwaka 2001 aliibeba Simba mpaka hatua ya makundi
ligi ya mabingwa barani Africa mbele ya Zamalek ya Misri.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako