Friday 21 September 2018

JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA

Nguli wa Muziki wa Reggae nchini Tanzania Samwel Mleteni maarufu kwa jina la Jah Kimbute amefariki jana nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam
Jah Kimbute
Mwili wa Marehem unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Jijini Tanga kwa maziko.

MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU BARA MZUNGUKO WA TANO


Friday 7 September 2018

KAMPENI YA FURAHA YANGU

VIONGOZI WA SERIKALI NA WADAU WA KAMPENI YA FURAHA YANGU

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MY WAY TANZANIA

ZOEZI LA UPIMAJI LIKIENDELEA MBAGALA ZAKIEM
MKUU WA WILAYA YA TEMEKE MHE FELIX LYANIVA AKIPITA KWENYE MABANDA YA UPIMAJI

Monday 23 October 2017

ZIARA YA NAIBU WAZIRI SHONZA

NAIBU WAZIRI WA HABARI JULIANA SHONZA KUSHOTO AKIPATA MAELEKEZO KUTOKA KWA VIONGOZI WA TBC


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amewaasa wanahabari kutumia vizuri taaluma yao katika kutoa habari zenye weledi zinazoleta manufaa kwenye jamii na kusisitiza kuwa endapo taaluma hiyo ikitumika vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa jamii.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika makao makuu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) barabara ya TAZARA jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Shonza amesisitiza ushirikiano kati ya serikali na wanahabari ili kuipeleka mbele zaidi taaluma ya habari nchini.
Vile vile Naibu Waziri Shonza ameipongeza TBC kwa kuwaamini vijana na kuwapa fursa kubwa ya kufanya kazi na kuendana bega kwa bega na sera ya serikali inayosisitiza kutoa nafasi nyingi kwa vijana katika kulitumikia taifa.
Amesema anashukuru sana kwa ushirikiano aliopewa na TBC na kusisitiza kuwa kwa kushirikiana na Waziri Mwenye dhamana ya wizara hiyo wanashughulikia changamoto zote zinazolikabili shirika hilo.
Ameipongeza TBC kwa kuwa mfano bora miongoni mwa vyombo vingi vya habari nchini na kuviasa vyombo vingine kufuata misingi bora ya taaluma ya habari.
NAIBU WAZIRI AKIWA NDANI YA STUDIO ZA TBC INTERNATIONAL
Hii ni ziara ya kwanza kwa Naibu Waziri Shonza kufika TBC tangu alipoteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli Oktoba saba mwaka huu akichukua nafasi ya Anastazia Wambura.
NAIBU WAZIRI SHONZA ALIPOTEMBELEA STUDIO ZA TBC FM
Habari/picha
Hamisi Hollela na Mahmud Rajab

Wednesday 19 April 2017

NU TRACK

BRAND NEW Track!!!
BADtaito jr Xplastaz & Mstaafrika Presents;
Track: LIVE DIMBANI
Artists: Killa X Gp-Rowdix
Prodution: NOIZMEKAH Arachuga
Genre: Hiphop Asilia
Kupakua wimbo huu mkito BOFYA HAPA

👇🏽👇🏽👇🏽
https://mkito.com/song/16344

#Video Coming Soon.
#Follow Facebook Pg.
@BADtaito jr Xplastaz
@Mstaafrika Arts Music & Culture, Tanzania
Whatsapp: +255758510605
#Support Indigenous Hiphop Tanzania
#BuildersLaneMusic
#EastAfricaCollectiveMovement.
Song Dedicated to all warriors fighting to Expose & Explore real Hiphop worldwide.

Friday 14 April 2017

MBADALA WA BABU WENGER

London, England .Arsenal imeanzisha mazungumzo na kocha wa Juventus, Max Allegri wakati hatima ya Arsene Wenger ikiwa njia panda.
Gazeti la SunSport limebainisha kuwa Gunners imekuwa na mawasiliano na Allegri katika siku saba zilizopita katika kuangalia uwezekano wa kumchukua Mtaliano huyo kushika mikoba ya Wenger.
Hivi karibuni kiongozi moja wa Arsenal alikuwa hafahamu kama Wenger ataendelea kubaki klabu hapo, wakati kocha huyo akiendelea kupata matokeo mabovu na kuongeza shindikizo kutoka kwa mashabiki.
Pia, kuna taarifa kuwa klabu hiyo inahitaji mkurugenzi wa ufundi na winga wa zamani wa klabu hiyo Marc Overmars ametajwa kujaza nafasi hiyo.
Hata hivyo, Wenger anajua kuwa kuna mambo yanayoendelea nyuma yake.
Mwenendo wa kusuasua wa Arsenal kwa sasa umewalazimisha viongozi kumfuatilia Allegri ( 49) mwenye mafanikio makubwa kwa sasa.
Mtaliano huyo ametwaa ubingwa wa Serie A na Kombe la Italia katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Juventus na sasa pia yuko katika nafasi nzuri ya kutwaa taji msimu huu.
Jumanne iliyopita aliingoza Juventus kuichakaza Barcelona kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Jambo zuri zaidi ni kwamba Allegri mwaka jana alimaliza masomo yake ya Kiingereza akiwa ni maandalizi ya kuachana na miamba ya  Serie A na kutimukia Ligi Kuu England.
Kocha huyo pia alikuwa akitakiwa na Chelsea kuziba pengo la Jose Mourinho, lakini kwa bahati mbaya nafasi ikaangukia kwa  Antonio Conte

Friday 7 April 2017

KUTOKA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO

Taarifa rasmi kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo juu ya kutoweka kwa wasanii Roma Mkatoliki na Moni Central zone

WASANII ROMA , MONI KUTOKA CENTRAL ZONE NA WATU WENGINE WAWILI WATOWEKA

Wasanii wawili kutoka Tanzania Ibrahim Mussa ajulikanae kama Roma Mkatoliki na Moni pamoja na producer wa Togwe records Bin laden na Emma ambaye ni mfanyakazi wa mama mzazi wa mmiliki wa studio za tongwe records J Murder wametoweka katika mazingira ya kutatanisha wakiwa katika studio hizo za togwe baada ya kuvamiwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana katika gari aina ya noah;J murder ameeleza kushtushwa na tukio hilo na kuongeza kua watu hao walibeba baadhi ya vifaa vya studio na kuondoka navyo.
Baada ya tukio hilo mmiliki wa tongwe rec J Murder alifika kituo cha polisi cha Oysterbay na kuripoti juu ya tukio hilo.

Nae Nancy mke wake roma anaeleza kua simu ya mume wake inaita tu bila kupokelewa na hadi hivi sasa hajui mume wake yupo wapi.
Wasanii kwa umoja wao wameungana kuweza kufatilia swala hilo ambalo hadi hivi sasa hakuna anaejua wasanii hao wako wapi.

Thursday 6 April 2017

NEW TRACK MAUA SAMA

#BrandNewTzVideo Bofya bio ya @mauasama au HAPA https://youtu.be/CO9WYgaeFYg kutazama Official Video ya #MainChick na Pia unaweza kuirequest kwenye vituo vyote vya Tv na radio ..
#supportgoodmusic
#goodmusiclives

Video directed by @khalifan_khalmandro
Produced by @kinglufa
Mastered by #chizanbrain
B RECORDS
Cc @reyjons
@mohchidunga
#MAINCHICK
#InfoPoweredBy #KwanzaPromo #VipajiVMGAfrica @kwanzapromo @teamkaskazi kwanzanetworks.com @vipajivmgafrica @djhazuu djhazuu.com #SapotiNyumbani

NEW TRACK 2017

#BrandNewTzAudio Bofya bio ya @LordEyesmweusi ft @juma_jux au HAPA @mkitodotcom https://mkito.com/song/16272 kupakua wimbo wa #HelaYangu #HelaYanguNtaipataje produced by @kingluffa & @chizanbrain
#InfoPoweredBy #KwanzaPromo @kwanzapromo @teamkaskazi kwanzanetworks.com @djhazuupromo @djhazuu djhazuu.com #SapotiNyumbani

Sunday 20 November 2016

"HATUNA BAHATI" Mourinho

Kocha wa kikosi cha Mashetani wekundu,Munchester United,Jose Mourinho amesema kikosi chake ni kikosi kisicho na bahati katika ligi kuu ya Uingereza kufuatia sare ya bila kufungana 1-1 na Washika bunduki wa Anfield Arsenal."Ninajua vijana wangu wanachukulia kama wamepoteza,wakati arsenal kwao ni kama ushindi"Mourinho.
Katika mpambano huo arsenal walisawazisha dakika ya 89 kupitia kwa Giroud na kufuta matumaini ya ushindi kwa united ambao walitangulia kwa bao safi la Juan Mata.

                                                      Jose Mourinho.       Picha kwa msaada wa Mtandao       





Monday 15 August 2016

MECHI ZA EPL WEEKEND HII

LIVERPOOL PLAYER COUTINHO
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema ushangiliaji wake pamoja na wachezaji wa Liverpool baada ya ushindi dhidi ya arsenal hauruhusiwi.
Katika mchezo wa ligi kuu ya england uliochezwa jioni ya jana jijini London, wenyeji wa emirates arsenal waliangukia pua baada ya kupata kipigo cha magoli 4-3 kutoka kwa majogoo wa anfield Liverpool.
Liverpool iliyochini ya klopp imeanza kampeni ya kusaka ubingwa wa epl kwa ushindi mnono licha ya arsenal kutangulia kufunga katika kipindi kwanza kupitia kwa goli lililofungwa na theo Walcott katika dakika ya 31 lakini kabla kipenga cha mwamuzi kupulizwa kuashiria kipindi cha kwanza kumalizika philipe coutinho aliisawazishia Liverpool kupitia mkwaju wa mpira wa adhabu ulizama wavuni katika dakika ya 45.
Katika kipindi cha pili Liverpool waliongeza idadi ya magoli dhidi ya wapinzani wao ambapo katika dakika ya 49 adam lallana aliukwamisha mpira wavuni kabla ya coutinho kurejea tena wavuni katika dakika ya 56 na saido mane kushindilia msumari wan ne katika dakika ya 63.
Arsenal walikusanya nguvu na dakika moja baada ya goli la mane, alex oxlade chamberlane aliifungia arsenal goli safi akiivuruga safu ya ushambuliaji ya Liverpool na calum chambers akifunga la tatu katika dakika ya 75.
 “sikupaswa kushangilia goli la nne wakati ilibaki nusu saa nzima. Nilifahamu kwa wakati ule lakini nilishachelewa”.
Aidha klopp amesema kilichomfurahisha zaidi katika ushindi huo ni namna ambavyo walitulia na kujilinda katika kipindi cha dakika 30 za mwisho ambapo arsenal walizidisha mashambulizi na hata kupelekea kuonekana huenda isingekuwa siku yao kushinda.
Upande wa pili wa shilingi mambo si shwari kwa kocha wa arsenal arsene wenger ambaye kikosi  chake kinazidi kuandamwa na majeruhi. Pamoja na kipigo cha ufunguzi asrenal imepata pigo la majeruhi baada ya mshambuliaji kinda wa timu hiyo alex iwobi kupata majeraha sambamba na kiungo aaron ramsey ambao walilazimika kutolewa nje kabla ya mechi kumalizika.
Kwa upande wake Kocha wa Manchester united Jose Mourinho ameelezea kufurahishwa na kiwango alichokionyesha kiungo Juan mata baada ya kufunga goli katika mchezo wao dhidi ya Bournemouth.
Mata alifungua ukurasa wa magoli wa united msimu huu baada ya kupachika goli dakika 5 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na kuipa uongozi united katika dimba la vitality, kabla ya wayne rooney na Zlatan Ibrahimovic kuongea mengine mawili katika kipindi cha pili.
Adam Smith aliifungia Bournemouth goli la pekee lakini kikosi hicho cha mourinho kilipigana kuwazuia Bournemouth kuongeza mengine mpaka mpira kumalizika na kujinyakulia pointi tatu muhimu.
Mata ambaye aliuzwa united na mourinho alipokuwa Chelsea alifanyiwa mabadiliko ya kutolewa nje baada ya kuingia uwanjani katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Leicester na sakata hilo kuleta mtazamo tofauti baina ya mashabiki wa united lakini mourinho ni kama aliwajibu mashabiki hao kwamba hakuna kitu yao na kuamua kumuanzisha mata katika mchezo wa jana na mourinho kusema ilikuwa mechi sahihi kwa mata kuonyesha kiwango chake.
“lilikuwa goli muhimu lenye kutumia akili, goli kutoka kwa mtu wa mpira. Namjua vizuri kwasababu nimefanya nae kazi kwa miezi sita tulipokuwa Chelsea, najua fika kipi anachoweza kutoa na kipi asichoweza”.
 Mourinho ameongeza kuwa anafuraha kwa mata lakini pia anafuraha kwa timu nzima hata wale waliokuwa nje na kuingia kutoa mchango wao katika ushindi na hata wasiopata nafasi ya kucheza kwani wote kwa pamoja wanajenga familia moja.
Mechi inayofuata united watawakaribisha Southampton old Trafford na mourinho kuwa na mtazamo chanya kuelekea mchezo huo hasa baada ya kupata ushindi mfululizo.
@@@@@@@@@@@@@
Nae kocha wa Manchester city, pep guardiola amekiri kwa mlinda mlango wake joe hart kuchukizwa kwa kuachwa katika kikosi cha man city wakati timu hiyo ikianza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya epl.
Mara baada ya kuteuliwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo, guardiola hakuchelewa kubadilisha baadhi ya vitu ikiwa ni sambamba na kumuacha mlinda mlango huyo ambaye si tu chaguo la kwanza kwa klabu ya man city lakini pia ni mlinda mlango nambari moja wa timu ya taifa ya England.
Hart aliishuhudia timu yake siku ya jumamosi ikishinda magoli 2-1 dhidi ya sunderland akiwa nje na kitendo hicho kuibua tetesi za mlinda mlango huyo kutimka city.
Guardiola amesema ana uhakika kwamba hart amechukia, lakini si kila mchezaji asiyepata nafasi katika kikosi kitakachoanza atauzwa bali amesema kuwa anatakiwa achague timu na kwa sasa ana wachezaji 28 na kati ya hao wanatakiwa wamshawishi zaidi uwanjani.
Licha ya kuwa na msimu mzuri 2015/2016 na kuwa mchezaji muhimu wa man city katika miaka ya hivi karibuni lakini kushindwa kuonyesha makali katika michuano ya kimataifa ya euro mwaka kumeifanya klabu ya man city kuhusishwa na kutaka kusajili magolikipa wengine huku taarifa hizo zikichagizwa zaidi na ujio wa pep guardiola.
Hata hivyo guardiola ametupilia mbali taarifa za kumshusha hart na kusema bado mlinda mlango huyo anaweza kuwa chaguo lake la kwanza na kutetea uamuzi wake wa kumuanzisha langoni willy caballero kwani muarjentina huyo alianza mazoezi mapema kabla ya joe hart.

@@@@@@@@@@@@@@@