Friday 26 July 2013

CESC FABREGAS AITAMANI MAN UNITED

                            
Kiungo Cesc Fabregas amewaambia rafiki zake kuwa anatamani kuondoka Barcelona na kuhamia Manchester United.

Kiungo huyo wa Hispania kwa sasa anagombewa na United na Barcelona, na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamekwisha toa ofa ya Pauni Milioni 30
Kocha wa UNITED David Moyes aliwambia waandishi wa habari nchini Japan Jana kuwa mpango wa Club hizo kufanya biashara ya Nyota huyo wa zamani wa Arsenal unaendelea na ofa nyingine itatolewa endapo Cecs ataamua kuomba kuondoka Barca mambo yanaweza kubadilika
 

Van Persie anatarajiwa kucheza sehemu kidogo baada ya kupata ahueni ya maumivu yake, wakati Moyes pia amesema kwamba Nahodha wake, Nemanja Vidic — ambaye pia amekuwa majeruhi ameanza kucheza soka ya ushindani nyumbani England.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako