MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Maulid Ali ‘Maufundi’
amesema kuwa katika historia ya maisha yake hawezi kuigiza katika komedi, Mau
anasema kuwa hadhi ya Komedi imepotea baada ya kuibuka Komedi za kukurupuka na
kujikusanya na kurekodi bila ya kutumia muswada (Script) ambalo linaua sanaa
hiyo.
Maufundi akiwa location kurekodi filamu ya Chips
kuku.
“Ninajua thamani yangu siwezi kuigiza katika Komedi changanyikeni, hawa
ndio wanaotuharibia kwa kukurupuka na kurekodi vuluvulu, ndio maana komedi zetu
zinaanzia gengeni kuvaa nguo mbovu mbovu na kuwa wachafu, kila siku nawaambia
wachekeshaji wenzangu kuchekesha siyo lazima kuwa wachafu tunatakiwa kubadilika
kuwa smart,”anasema Mau.
Msanii huyo ambaye kwa mwaka huu amekuwa gumzo katika tamasha la filamu
la kimataifa la ZIFF kwa kuonyesha filamu yake ya Chips kuku iliyotikisa Ngome
Kongwe, alisema kuwa mbona wasanii kama Martin Lawrence, Fresh Prince Queen
Latifa na wengineo wanachekesha huku wakiwa nadhifu, naye anakuwa kama hao.
Lakini jambo lingine ambalo linamfanya ashindwe kuunga na wachekeshaji wengine
ni maslahi, kutokana na watayarishaji wengi wa komedi kudharauliwa na kulipwa
fedha kidogo wakati wao ni kipenzi cha watazamaji wengi, Mau kawahimiza
wachekeshaji kubadilika na kuwa na misimamo kwa ajili ya fani yao, pia Mau
anasema wasanii wengi kufungia kama Ng’ombe na kuigiza kwa pamoja inaua sanaa
hiyo, kwanii kila mtu anataka kumfunika mwezake.
SOURCE: Filam Central Tanzania
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako