Friday 28 March 2014

PICHA 20 ZA MVUA ILIVYOLETA SHIDA JIJINI DAR ES SALAAM NA MIKOANI LEO

 
 

MUONEKANO MPYA WA DIAMOND PLATNUMZ


OMMY DIMPOZ AENDELEA KUFANYA KWELI



Ni zamu ya staa wa bongofleva anayetajwa kuwa wa pili kwa kupokea malipo makubwa kwenye show mbalimbali anazozifanya (milioni nane kwa show za ndani ya nchi).
Siku kadhaa baada ya kutua Tanzania akitokea Marekani na Uingereza alikokwenda kufanya show pia, Ommy Dimpoz amepata dili jingine zuri kwa kualikwa kuimba na band yake aliyotoka nayo bongo katika party ya kampuni ya mafuta huko Muscat Oman.
Kwa siku kadhaa Ommy ambae ni miongoni mwa vijana wachache wa bongofleva wanaosifika kwa kujituma na kuwa serious na kazi, alionekana akifanya mazoezi na band yake ambayo ndio atahusika nayo mwanzo mwisho kwenye stage Leo Ijumaa March 28 2014

Thursday 27 March 2014

RAIS KENYATTA ASIMAMISHA MSAFARA WAKE NJIANI KUPATA CHAKULA CHA MCHANA



Vituko vya mara kwa mara haviishi kwa Raisi wa Kenya, Bwana Uhuru Kenyatta, ambapo wiki hii wakati alipotoka kwenye mkutano wake yeye na marais wengine aliamua kusimamisha msafara wake na kupata chakula cha mchana eneo la kawaida kabisa.
Tukio hilo limewashangaza wengi ambao walikuwa wakishangaa msafara huo wa Rais ukipita mara ghafla ukakata kona na kupaki pembeni na waheshimiwa kushuka kupata mlo wao wa mchana kwenye eneo liitwalo Kaijado tena chini ya mti.
Walioshuka kupata chakula cha mchana ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto pamoja na wasaidizi wao.
Rais Kenyatta anaonekana kuwa karibu na kutaka kuishi maisha ya kawaida tofauti na yale ya waheshimiwa maraisi wa nchi zingine, ambapo wiki iliyopita video moja ilimuonyesha akinunua karanga kwa muuzaji anayetembeza mtaani.
Hakuishia hapo pia aliwahi kutembea jijini Nairobi bila msafara kama ilivyozoeleka hadi Trafiki akamshangaa aliporuhusu gari za upande huo na kumuona akiwa anaendesha gari hizo ambazo alizisimamisha kwa muda kidogo.

Wednesday 26 March 2014

CHAMELEONE PESA NYINGI HADI ANAHESABU KWA MASHINE


Mkali wa nyimbo ya Tubonge kutoka Uganda, Jose Chameleone ambaye ni mmoja kati ya wanamuziki wa Afrika anayetajwa kuwa ana utajiri mkubwa sana, ameonyesha jeuri ya pesa kwa kuzihesabu kwa kutumia mashine.
Kwenye hii picha Jose Chameleone anaonekana akitumia mashine ya kuhesabia pesa akizihesabu dola mia za kimareakani zikiwa kwenye mafungu makubwa ndani ya begi.

Zaidi ya pesa hizo pia Chameleone anamiliki nyumba ya kifahari, magari kama Escalade na mengine pamoja na vitega uchumi.
Chameleone kama anavyojiita, Dr Mayanja anapata kiasi kikubwa cha pesa kwa kufanya matamasha sehemu mbalimbali duniani pamoja na kuandaa yake binafsi.

Kama wiki hii ameandaa tamasha kubwa ambalo amelipa jina la Tubonge East African concert linalotegemewa kushirikisha wasanii wa africa mashariki na hadi sasa limeshadhaminiwa na makapuni makubwa ya Uganda.

CHEKI TATOO KUBWA ALIYOCHORA JUSTIN BEIBER MKONONI



Justin Bieber anaonekana kutaka kujibadili kabisa kwa vitu mbalimbali tofauti na Yule tuliyekuwa tunamjua kwenye Albam yake ya My World na wimbo kama Baby.

Jarida la forbes ya over exposed celebrity,la hivi karibuni Justin Bieber alikaa top kwenye hiyo list kutokana na matukio yake ya kukamatwa na polisi pamoja na kuamua kubadilisha muonekano wake kabisa kwa kuchora tatoo kubwa kwenye mikono yake yote miwili.

Bieber ana tatoo kadhaa kwenye mwili wake ambazo zilikuwa hazionekani kutokana na nguo lakini hizi zitakuwa zinaonekana vizuri kwa sababu zipo mikononi na rangi yake inaruhusu tatoo kuonekana vizuri.

Tuesday 25 March 2014

MAONI YA MASANJA MKANDAMIZAJI JUU YA HUSBAND NA WIFE MATERIAL


WANAOWANIA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2014 HAWA HAPA



Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi yaani ‘nominees’ wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania.
Kabla ya kuanza kutajwa kwa wanaowania tuzo za KTMA 2014, BASATA ilitangaza nyimbo ambazo zimetolewa kwenye kuwania tuzo hizi kutokana na sababu za kimaudhui, Uzuri wako yake JUX, Nimevurugwa yake Sunra wa Majanga na Tema mate tuwachape yake Madee

 
 
 
 
 
 

Kuna hizi Zingine ambazo ni
WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI
Tubonge ya Jose Chameleone,
Nakupenda pia ya Wyre na Alaine, 
Badilisha ya Jose Chameleone, 
Kipepeo ya Jaguar, 
Kiboko changu ya Amani, Weasal na Radio.

WIMBO BORA WA TAARAB – 
Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, 
Asie kujua hakuthamini Isha na Saida Ramadhani, 
Nipe stara Rahima Machupa, 
Sitaki shari Leila Rashid, 
Fahari ya mwanamke ya Khadija Kopa, 
Mambo bado Khadija Yusufu,
Kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.

WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL – Nishai ya Chibwa ft Juru, 
Sexy Lady ya Dr. Jahson, 
My sweet ya Jettyman Dizano, 
Feel alright ya Lucky Stone na
Wine ya Princess Delyla.

WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA – 
Muziki gani ya Ney wa Mitego ft Diamond, 
Joto hasira ya Lady Jaydee ft Prof J,
Kidela ya Ally Kiba na Abdu Kiba, 
Bila kukunja goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na Tupogo ya Ommy Dimpoz ft J Martins.

RAPA BORA WA MWAKA WA BENDI – Kitokololo,
Chokoraa, 
Ferguson, 
Canal Top na 
Totoo ze bingwa.

MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI – 
Khadija kopa, Vanessa Mdee, 
Isha Ramadhani, Luiza Mbutu, 
Catherine (Cindy)

MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA TAARAB – 
Enrico, 
Ababuu mwana wa Zanzibar na 
Bakunde.

MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA (BENDI) – 
Allan Mapigo, 
C9 Kanjenje, 
Enrico, 
Amoroso na 
Ababuu mwana wa Zanzibar.

WIMBO BORA WA REGGAE – 
Niwe nawe ya Dabo, 
Hakuna matata ya Lonka, 
Tell me ya Dj Aron ft Fidempha, 
Bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P & Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors from the east.

WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA
Kwejaga nyangisha ya Batarokota, 
Nalonji ya Kumpeneka, 
Bora mchawi Dar bongo massive, 
Tumbo lamsokota ya Ashimba, 
Aliponji ya Wanakijiji na 
Agwemwana ya Cocodo african music band