Friday 26 July 2013

DIAMOND PLATINUM AENDA AFRIKA KUSINI KUREKODI VIDEO YAKE MPYA

Msanii anayependwa na mashabiki wengi wa muziki wa Bongoflava nchini na Afrika kwa ujumla Nassib Abdul maarufu kama Diamond yuko nchini Afrika Kusini akirekodi video yake mpya kabisa.
Taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani na vya kuaminika zinasema kuwa Diamond ameondoka hivi karibuni kwenda kurekodi video hiyo ya wimbo unaojulikana kama "Tumetoka Mbali" ambao inasemekana amemuimbia mke wake mtarajiwa Penniel Mwingila anayejulikana kwa jina la DVJ Penny mtangazaji kutoka Television ya DTV.
Diamond amekwenda Afrika kusini kufanya video hiyo na Kampuni maarufu ndani ya Afrika Mashariki yenye maskani yake Nchini Kenya inayoitwa OGOPA, na vifaa vinavyotumiwa kurekodia video hiyo ni vya kisasa. (punde tutaweka picha za video hizo)
PATAPICHA ilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kwenye simu zake za kiganjani zaidi ya nne ila zote hazikupatikana, hata ile line yake maalum ya Airtel nayo haikupokelewa.
Jitihada hazikuishia hapo PATAPICHA ilimtafuta mke mtarajiwa wa Diamond, Penny ili kujua ukweli wa mambo, alipopigiwa simu ilipatikana na maongezi yalikuwa hivi.

PATAPICHA: Hallow Peniel Mwingira
PENNY: Kimya
PATAPICHA: Hellooooooooow Peniel Mwingira 
PENNY: Yees ni Penny Mwingila
PATAPICHA: Okey Peniel Mwingila, mimi natoka PATAPICHA Blog
PENNY: Patapicha nini 
PATAPICHA: PATAPICHA Blogspot 
PENNYOkey niambie
PATAPICHA: Kuna habari zimetufikia kutoka kwa chanzo cha ndani ya kuwa Diamond amekwenda kurekodi video ya wimbo unaoitwa Tumetoka mbali ambao amekuimbia wewe, Tupe undani wa taarifa hizi
PENNYmmhhhh Mimi kwa kweli sifahamu, sifahamu kabisa kama amekwenda kurekodi video labda umuulize mwenyewe anaweza akakupa jibu
PATAPICHA: Okey tumejaribu kumpigia kwenye line zake zote hapatikani na ya Aritel hapokei simu
PENNY: Yaaa msubiri akipokea umuulize maana mimi sina jibu la kukupa, I'm sorry
PATAPICHA: Okey penny tunashukuru
PENNYthanks, but very sorry

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako