Saturday, 6 July 2013

SABA SABA NA TAMASHA LA MATUMAINI

Tamasha la Matumaini linatarajiwa kufanyika siku ya saba saba katika uwanja wa Taifa huku kukiwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wabunge na wasanii mbalimbali.

Kwa wale wapenzi wa ndondi kutakuwa na mapambano kati ya Thomas Mashali wa Tanzania dhidi ya Patric Amote kutoka Kenya huku Fransis Miyeyusho akipambana na Shedrac Machange kutoka Kenya
 Francis Miyeyusho akiongelea pamabano lake na Shedrack Muchanje kutoka Kenya
 Thomas Mashali akizungumza namna gani atamtwanga mpinzani wake Amote kutoka Kenya

Vile vile kutakuwa na Mapambano ya utangulizi ni kati ya Mhe Idd Azzan (MB) Ilala vs Jacob Steven (JB) huku Jackline Wolper  akipambana na Mhe Halima MDEE (MB) Kawe na Mhe Zito Kabwe vs Ray Kigosi
                                               JACKLINE WOLPER MASSAWE
                JB AKITAMBA KUMTWANGA MPINZANI WAKE KWENYE ROUND YA KWANZA
   Mhe IDD AZZAN "Mimi sina maneno mengi sababu mimi sio msanii"
                                                           Mhe Zitto Kabwe
                                               Ray Kigosi katikati
                                                Halima Mdee akiwa mazoezini
Viingilio vitakavyopatikana kwenye Tamasha hilo la Matumaini vitakwenda moja kwa moja kwenye sekta ya elimu hayo yamesemwa na  Mratibu wa TAMASHA hilo Abdallah Mrisho (Abby Cool)

Kutakuwa na mechi ya Wabunge ambayo inatarajiwa kuongozwa na Mhe Jakaya Kikwete na Wasanii wa Bongo movie watacheza na Wasanii wa Bongo fleva huku wasanii kutoka TMK Sir Nature ,Tandale Diamond na Kenya Prezoo watakuwepo kutoa burudani kwa watanzania
                                Alex Msigala Afisa Masoko wa tiGO kampuni ya simu za mkononi
             Mbunge wa Igalula Dkt Mfutakamba (Timu ya wabunge upande wa Yanga)
              Mbunge wa Nzega Dkt Hamisi Kigwangala (Timu ya wabunge upande wa Simba)
           Abdallah Mrisho maarufu kama ABBY COOL mratibu wa Tamasha la MATUMAINI
                                          Diamond kushoto akiwa na H- BABA

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako