Friday, 26 July 2013

AJALI YA TRENI SPAIN ILIYOUA WATU WENGI NA KUACHA MAMIA YA MAJERUHI

DEREVA WA TRENI ILIYOPATA AJALI

Dereva wa treni iliyoua watu zaidi ya 80 anadaiwa kujisifia kwa kuendesha treni kwa kasi kupitia ukurasa wake wa Facebook kabla ya ajali hiyo kutokea.
SPEED MITA YA TRENI ILIYOPIGWA PICHA IKICHUKULIWA KWENYE UKURASA WA FACEBOOK WA DEREVA HUYO ALIYEPOST KUONESHA JINSI ANAVYOENDESHA KWA KASI
Fransisco Jose Gardon anasemekana kuposti picha ya mwendokasi wa treni unaoonesha treni hiyo ikikimbia kilomiota 125 kwa saa.
BALAA TRENI IKIWA CHINI NA WATU NDANI INASIKITISHA SANA
BAADHI YA MAJERUHI WA TRENI WALIOOKOLEWA  WAKIELEKEA HOSPITALI MARA BAADA YA KUPEWA HUDUMA YA KWANZA

Ingawa ukurasa huo ulifutwa mara baada ya kutolewa katika gazeti la kihispaniola; hata hivyo jaji wa mahakama ya Galcia amewataka police kuchukua maelezo kwa dereva huyo ambaye yuko chini ya ulinzi katika hospitali moja nchini humo.
ASKARI WA UOKOAJI WAKIWA KAZINI
MAJERUHI AKIWA HAJIWEZI MARA BAADA YA KUOKOLEWA KUTOKA KATIKA MABEHEWA YA TRENI
Waziri mkuu wa Uingereza ametoa taarifa yake kwa raisi wa Spain kwa kuwapa pole ndugu wa marehemu pamoja na majeruhi.
MAJANGA
ASKARI WA UOKOAJI WAKIOKOA WAHANGA WA AJALI HIYO

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako