Tuesday 16 July 2013

PREZZO AKATAA KUMUOMBA MSAMAHA DIAMOND KWENYE TWITTER


 
Lile sakata la majibishano ya maneno kati ya wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya kutoka Afrika ya Mashariki limeendelea kushika kasi.
Baada ya Diamond kudai amepigiwa simu na Prezzo kuomwa msamaha kutokana na tweet alizotumiwa wiki iliyopita, Mwanamuziki Prezzo kutoka Kenya amesema hawezi kamwe kumuomba msamaha Diamond kupitia Mtandao wa twitter kwa kuwa hilo ni jambo la kitoto.
“Mimi sipendi kuwa na adui kwa sababu muziki unafaa kuleta muungano, sa mi nikashangaa mbona huyu brother ananiingilia na huku sikumbuki kumkosea wala hatujawai kukutana ana kwa ana” Prezzo ameongea maneno hay oleo mchana kwenye kipindi cha Mambo mseto cha Radio Citizen.
Aliongeza ya kuwa Diamond ndiye aliyemchokoza baada ya wasanii hao kutumbuiza mwanzoni mwa mwezi huu kwenye Tamasha la Matumaini, kasha Diamond kumponda yeye kwenye Gazeti mojawapo la Udaku nchini Tanzania ya kuwa hamwezi kwa lolote kwenye muziki huu.
“Mtu yeyote anamjua Prezzo kama Rattle Snake, ukimchokoza tu you have to get prepared to be bitten”
Prezzo aliendelea kusema kwamba alimpigia simu Diamond lakini hakupokea na ndio maana aliamua kum-diss kwenye mtandao wa Twitter.
“Jamaa hakupokea simu nikaona aahh!! Basi liwalo na liwe, nika-decide ku-air my views”
Hata hivyo Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kama anavyotaka afanye.
“Unaona kwa saa hizi akianza kusema niende kwa Twitter niombe msamaha, maisha hayakwendi hivyo….. kwa hiyo vitu vingine naona ni kama utoto, yeye kusema niombe msamaha kwa Twitter…. Niombe msamaha kwa kosa gani? Kusema kweli unajua mimi ni msema kweli na kuomba msamaha kwa Twitter naona ni utoto”
Pia Prezzo alimshukuru Mtangazaji William Tuva kwa kujaribu kuwasuluisha yeye na Diamond kwa kuwa yeye hapendi bef na wasanii wenzake.
Source: Radio Citizen na William Tuva kwenye Twitter

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako