Wednesday 21 August 2013

MJUE MTU MWENYE KILO NYINGI DUNIANI

Kijana Khalid bin Mohsen Shaari ndiye binadamu mwenye uzito kuliko wote duniani akiwa na uzito wa Paund 1,345 ambazo ni sawa na kilo 610. 
                             
Shaari ameshindwa kuinuka kuinuka kitandani takribani mwaka mzima kutokana na kuzidiwa kwa uzito wa mwili wake anatarajiwa kufanyika matibabu ya kumwezesha kurudi katika hali yake ya kawaida. 
 
Mfalme wa Saudi Arabia, ameingilia kati mpango wa kumsaidia Khalid bin Mohsen Shaari ambaye ni raia wa nchi hiyo, ambapo ameahidi kuchangia katika mchakato wa kumtibu na kumrudisha katika hali nzuri zaidi.
Kutokana na unene, ukubwa na uzito wake, Khalid hawezi kutembea wala kusogea mwenyewe bila msaada wa kifaa maalum cha kumbeba akiwa katika kitanda chake, na cha ajabu zaidi.
Ni kijana mdogo tu ambaye umri wake ni kati ya miaka 18 na 20.
Kwa mujibu wa rekodi za Guiness, Manuel Uribe kutoka Mexico ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mzito na mnene zaidi duniani ambapo alikuwa na uzito wa kilo560, Na baada ya kuonekana na kuingizwa katika matibabu, kwa sasa amepungua na kufikia uzito wa kilo 444.
Mfalme Abdullah tayari ametoa amri kuwa Khalid kuhamishwa huko Riyadh kwaajili ya mchakato wa matibabu yake.
Hapa alikuwa anapelekwa hospital kutoka nyumbani inabidi watumie Gari ya kuinua vitu vizito 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako