Monday 29 July 2013

DIMERA APATA JIKO JUMAMOSI

Mfanyakazi wa Clouds Media ambaye pia ni muigizaji maarufu nchini Tanzania Simon SImalenga Almaarufu kama Dimera Jumamosi ya wiki iliyopita alifanikiwa kufunga ndoa katika kanisa Katoliki Sinza, Parokia ya Mtakatifu Maria.
Bwana Harusi akiwa ndani ya Gari aina ya Benz kuelekea Kanisani kula kiapo kitakatifu
Harusi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group pamoja na wanafunzi wa Dar es Salaam School of Journalism (chuo ambacho walisoma bwana na Bibi harusi na kuanza uhusiano wao hapo).
 Simon Simalenga a.k.a Dimera akiwa na Mke wake Neema Inana 
Baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa hilo la Sinza, Tafrija imefanyika katika ukumbi wa Picoll Kawe 
Baadhi ya waliokuwa wanafunzi wenzao Bwana na Bibi Harusi (kutoka kulia ni Haji Mkali, Fat-hya Chambo, na Soudy Brown) 
 Bibi Harusi Neema Inana akiwa amepozi Saloon kusubiri kwenda kwenye tukio la Ndoa 
 Mfanyakazi wa Clouds Media Group Ephrahim Kibonde akiwa na Millenny Nafisa
 Waliokuwa wanafunzi wa DSJ kutoka kulia ni Jacob, Fat-hya, Soudy na Millenny
 Bi. harusi akiwa na wapambe wake wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa  
Simon Simalenga akiwa na Mke wake Neema Inana ndani ya Ukumbi wa Picoll - Kawe

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako