Friday 26 July 2013

STORI INAYOMHUSU KITALE KUTAFUNA MALI ZA SHARO MILIONEA



Msanii  wa  Comedy nchini na muimbaji wa bongo fleva  Kitale "Rais wa mateja", amekanusha taarifa zinazomuhusisha na mali za Marehemu Sharo milionea.
 MSANII KITALE MWENYE FULANA NYEUPE KATIKA MSIBA WA NGWEAR 

Katika  A/C yake ya BBM Kitale ameandika 
  "mama wa marehemu sharo Milionea ametoa malalamiko juu ya kutokabidhiwa baadhi ya mali za marehemu Sharo.
Waandishi bila kumuelewa mama sharo, wao moja kwa moja wananihusisha na mimi kuwa nahusika.  Hii ni kwa watanzania wote, Marehemu Sharo Milionea aliacha gari aina ya Opah, naomba kuwaambia watanzania ile gari haipo chini yangu, ile Gari ipo chini ya Muddy Suma, ambaye ni mwenye gari aliyopata nayo ajali Sharo na mama yake  Sharo kulalamika kwenye vyombo vya habari ni sawa na ni haki yake kwa sababu mwenye Gari aliahidi kusamehe, ila aliomba aachiwe mpaka atakaponunua gari nyingine. Kinachoshangaza sasa ni mwaka unakwenda gari haijauzwa wala nini  kwa hiyo mama anahisi mimi na Mudy suma letu moja.  Hapana mzazi wangu mimi nipo pamoja na wewe, na watanzania wote naomba muelewe gari sinayo mimi, maana kila muandishi ananiandama mimi. Kitu ambacho mimi na Sharo tulishea ni move tu. Gari anayo Mudy suma sababu  yeye  ndiye aliwezesha na kuhusu sofa anazo Mudy Suma"
KITALE AKISWA NA MAREHEMU SHARO ENZI ZA UHAI WAKE

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako