Friday 19 July 2013

KUONGEZWA UMRI WA KUOLEWA KWA WANAWAKE NCHINI GHANA

Imeelezwa Nchini  Ghana kuwa Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Ghana, Bi Philomena Nyarko, amesema umri halali wa mwanamke kuolewa unapaswa kuongezwa kutoka miaka 18 hadi 23.
Bi. Nyarko amesema, hatua hiyo itawafanya wanawake kujiandaa vyema kiakili na kimwili kuzaa watoto, na kwamba itapunguza ongezeko la idadi ya watu nchini Ghana kwa kati ya 15% hadi 20%.
JE NI KWELI WASICHANA WADOGO KAMA HAWA WATAKUWA WAMENUSURIKA KAMA RAI HIYON ITAKUWA SHERIA...NGOJA TUONE
Mapendekezo yake yamekuja wakati Wabunge nchini Nigeria wanajadili kuhusu kupunguza umri wa kuolewa kutoka miaka 18 ya sasa ili watu waweze kuoa na kuolewa katika umri mdogo zaidi.
Baadhi ya Wabunge Waislam, wametoa hoja kwamba, kuzuia watu kuolewa kabla ya miaka 18, unakiuka sheria za Kiislam ambazo zinaruhusu ndoa katika umri mdogo.
Nigeria ambayo inaongoza kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, imegawanyika kati ya Waislam na Wakristo.
WASICHANA WADOGO WANAOLEWA NCHINI GHANA NGOJA TUONE KAMA SHERIA ITALETA TIJA
Bi. Nyarko amesema kwamba, wanawake wanaochelewa kuolewa ama kuzaa hadi umri wa miaka 23 wanakuwa na afya njema.
“Inafahamika vizuri kwamba, matokeo ya afya njema kwa mama na mtoto, endapo atachelewa kuzaa hadi msichana anapokuwa amekomaa vya kutosha kwa ajili ya kuolewa na kubeba mimba ili kuokoa maisha ya mama na mtoto”, amesema Bi. Nyarko.
NA HAWA WASHIKA MILA JE? .......NGOJA TUONE

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako