Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu mwenye suti akipewa maelezo na afisa wa maliasili juu ya gari lililotengenezwa kwa miti ambalo linawavutia wengi bandani hapo |
GARI ya
mbao iliyobuniwa na mkazi wa kijiji cha Nyololo mkaoni Iringa, Keneth Mwangoka
imeokoa shilingi Bilioni moja kwa mwaka kwa kuhamasisha kuhifadhi mazingira
katika msitu wa Sao Hill ulioko mkoani humo.
Akizungumza
na MAELEZO katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
jana, Afisa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka Msitu wa Sao Hill
mkoani Iringa, Fidelis Mwanalikungu alisema gari hiyo ilibuniwa kwa
kushirikiana na Kikundi cha Sanaa cha Imehe kilichopo katika kijiji cha Nyololo.
Alisema
kikundi hicho kwa kutumia gari hiyo ambayo huvutia watu kuiangalia,
kinaeleimisha vijini 58 vinavyozunguka msitu wa Sao Hill kudhibiti matumizi ya
moto unawashwa na wakulima wakati wa kuandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo.
Alifafanua
kuwa uhamasishaji huo umefanikiwa kupunguza moto kutoka matukio 143 yaliyokuwa
yanasababisha hekta za misitu 500 hadi 1000 kwa mwaka hadi kufikia matukiio
manne tu kwa mwaka yaliyounguza hekta 17 za misitu.
“Ukiweka
hizo hekta 500 hadi 1,000 katika thamani ya fedha unakuta tulikuwa tunapoteza
kuanzia Milioni 840 mpaka Bilioni moja kwa mwaka kutokana na kuungua kwa msitiu
huo, sasa hii ni hasara kubwa” alisema Mwanalikungu.
Alisema
kutokana na elimu inayotolewa kushirikisha kikundi hicho, wameweza kuhifadhi
zingira ya msitu huo wa asili wa Serikali, vyanzo vya maji na kuhifadhi
mazingira ya vijiji hivyo.
Aliongeza
kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2009 uliobaini kuwa kutoka mwaka
2010 kurudi nyuma miaka 11 kulikuwa kuna matukio mengi ya moto yenye wastani wa
matukio 143 kwa mwaka.
“Ilipofika
mwaka 2011 tukaangalia ni mikakati gani tunaweza kuichukua kwa kuwashirikisha
wanavijiji, ndipo tukagundua wazo la kusema tukiwa na gari kama hili
linalovutia watu, tukaweka mabango ya kuelimisha tunaweza kufikisha ujumbe kwa
urahisi zaidi” alisema Mwanalikungu.
Akizungumzia
gari hiyo, Keneth Mwangoka gari hiyo aina ya Toyota Hiace aliinunua
kutoka kwa mtu ambaye alitaka kuiuza kama chuma chakavu na aliitengeneza ili
iweze kusaidia katika kuwavutia wanajiji na kupata njia ya kuwapata kwa
urahisia wanakijiji a kufikisha ujumbe.
Mwangoka
ambaye ni fundi wa gari hiyo, alisema gari hiyo ina injini ya Toyota 1S, robu
tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao na inatumia mafuta lita moja kwa kilomita
nane.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako