Thursday 25 July 2013

RAIA WAKIJESEVIA MAZIWA BAADA YA KONTENA KUTAKA KUPINDUKA UBUNGO




Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam walipata wasaa wakujihudumia maziwa ya Tanga Fresh mara baada ya Kibin (kichwa) cha Lori lililobeba Kontena la Maziwa hilo kuchomoka na kuacha njia maeneo ya Ubungo Mataa likitokea Jijini Tanga.
Ilikuwa kama ngekewa pale raia walipoona maziwa yanamwagika kutoka kwenye kontena na kutumia muda wao kukinga maziwa hayo kwa mahitaji ya nyumbani  na wengine kwenda kuuza kwa watu wengine bila kujali yana usalama kiasi gani.
Polisi walifika eneo hilo lakini teyari huduma ilikwishafanyika vilivyo na watu kuondoka na ndoo pamoja na madumu ya Maziwa Tanga Fresh. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyeripotiwa kujeruhiwa labda tu kwa wale watakaokunywa maziwa hayo na kuwaletea madhara baadae.




No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako