Nchi ya Ubelgiji jana Jumapili
imepata Mfalme Mpya wa 7 baada ya mzee wake Mfalme Albert kutawala kwa kipindi
cha miaka 20.
Mfalme Prince mwenye umri wa
miaka 53 ameapishwa jana kuwa mfalme mpya wa nchi ya ubeligiji Mfalme Philippe
sasa anachukua kiti hicho cha kifalme kutoka kwa baba yake mfalme Albert II
(79) ambaye amejiuzulu kutokana na sababu za kiafya.
Mtawala mpya wa Ubelgiji King
Philippe mwenye umri wa miaka 53 ameapishwa bungeni Julai, 21 2013 kwa kufuata
katiba ya nchi hiyo
“naapa kwa heshima ya katiba na
sheria za watu wa ubelgiji, kuwa nitalinda uhuru wa nchi hii na kulinda mipaka
yake” Mfalme Philippe ameyasema hayo kwenye kiapo chake
Ameongeza kuwa baba yake
ametawala kwa muda wa miaka 20, ameweza kutawala kwa kujiamini na kutekeleza
yote kwa upendo na umoja na kwa upande mwingine alikuwa makini na kutekeleza
majukumu kiuaminifu.
Wakishangilia siku ya uhuru wan
chi yao, wabelgijia wamejumuika kwa pamoja kwenye sherehe za kuapishwa kwa
mfalme wao mpya.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako