Monday 29 December 2014

MECHI YA AZAM NA YANGA


Klabu ya Dar Young African yenye makazi yake Jangwani Jijini Dar es salaam imelazimishwa sare ya goli 2 kwa 2 na Wana Lamba lamba Azam Fc katika uwanja wa Taifa hapo jana

Clab ya Azam ilikuwa ya kwanza kuona lango la Yanga mnamo dakika ya 6 pale Mbuyu Twite alipojichanganya na kipa wake Dida na kumpa nafasi Didier Kavumbagu kuamsha mashabiki wa Azam kwa shangwe
Lakin punde si punde furaha hizo zikazimwa na wana jangwani hao baada ya aliyekuwa mchezaji wa kulipwa wa simba Hamis Tambwe Hamis Magoli kutupia bao zuri la kichwa mnamo dakika ya 7
Mpaka muda wa mapumziko timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kwa goli kwa moja
Na kufanya mchezo kuwa wakuvutia zaidi pale tulipoona usajili wa mashabiki na mbwembwe zao uwanjani

Mnamo dk ya 52 Simon Msuva wa Yanga aliiandikia timu yake bao la pili na kuifanya Dar Yang AFRICAN kutawala mchezo huo, hadi ambapo
Azam waliamka na kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 64 bada ya kumtoa Salum Abubakar sure boy na kumwingiza Nahodha Jon Bocco Adebayo ambae hakufanya makosa mnamo dakika ya 65 alitupia mpira wa kichwa matata uliomshinda kipa shaban Dida na kutinga wavuni

Katika mechi hiyo timu ya Yanga iliwachezesha wachezaji wake wageni huku ikiwa ni mechi ya kwanza kwa kocha mpya Hans Van de pluijm

Yanga sasa inajiandaa kuumana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine kisha kuivaa timu ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Monday 15 December 2014

KISA CHA MAJOGOO YA ENGLAND KULALA KWA MASHETANI MEKUNDU

Kilabu ya Manchester United imeicharaza Liverpool mabao matatu bila majibu katika mechi ya kasi iliojaa mashambulizi makali kutoka pande zote mbili.
Hata hivyo ni Manchester United ndio walioona lango la Liverpool kupitia bao la nahodha wao Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza cha mchezo
Yuan Mata alifanya mambo kuwa mbili bila baada ya kufunga krosi iliopigwa na Young,bao ambalo wachezaji wa Liverpool walidhani ni la kuotea.

lakini Licha ya Liverpool kunoa safu yao ya mashambulizi na kuvamia ngome ya Manchester United kupitia Sterling aliyekosa mabao ya wazi Manchester united iliendelea kufanya mashambulizi kupitia Van Persie na Rooney.
Liverpool ilimuingiza Mario Balotelli ambaye pia naye alikosa mabao ya wazi huku Kipa wa Manchester akinyaka mashambulizi hayo.

Na baada ya dakika kadhaa Robin Van Persie alifanya mambo kuwa 3-0 baada ya safu ya ulinzi ya Liverpool kufanya masihara katika lango lao.
Liverpool sasa inajiandaa na mechi dhidi ya Arsenal katika mchezo unaofuata.

Thursday 11 December 2014

UEFA YATINGA MTOANO 16 BORA

MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA {UEFA} IMEENDELEA HAPO JANA KWA KUMALIZIKA AWAMU YA MAKUNDI NA KUTINGA RAUND YA MTOANO WA 16 BORA

KATIKA MECHI ZILIZOPIGWA HAPO JANA CLUB FC BARCELONA IMEWAFUNGA MAHASIMU WAO PARIS SAINT GERMAIN [PSG] GOLI 3 KWA MOJA KATIKA UWANJA WA NOU CAMP 
MAGOLI HAYO YALIWEKWA WAVUNI NA LIONEL MESSI DK 19, NEYMAR DK 42, NA SUAREZ DK 77, HUKU GOLI LA PSG LIKIWEKWA WAVUNI NA ZLATAN IBRAHIMOVIC

AIDHA KATIKA MECHI NYINGINE MANCHESTER CITY IMEFANIKIWA KUTINGA 16 BORA BADA YA KUIFUNGA AC ROMA GOLI 2 BILA
HUKU MABINGWA WATETEZI BAYERN MUNICHEN WAKIIFUNGA CSKA MOSKOW GOLI 3 BILA, CHELSEA NAYO IMEENDELEZA USHIND KWA KUIFUNGA 3 – 1 SPORTING LISBON
AJAX AMSTERDAM IMESHINDA 4 BILA DHIDI YA APOEL NICOSIA HUKU FC PORTO WAKITOKA SULUHU YA MOJA KWA MOJA NA SHAKHTAR DONETSK
TIMU ZILIZOFANIKIWA KUFUZU KWENYE RAUND YA MTOANO 16 BORA KUTOKA KUNDI A NI CLUB ATHLETICO MADRID NA JUVENTUS
KUNDI B NI REAL MADRID NA FS BASEL
WAKATI KUND C ZIKIPITA BORUSSIA DORTMUND PAMOJA NA ARSENAL
BAYERN MUNICH IMEFANIKIWA KUONGOZA KUND D IKIFUATIWA NA MANCHESTER CITY HUKU FC BARCELONA IKIVUKA AWAMU HIYO YA MAKUNDI NA PSG KUTOKA KUNDI E
CHELSEA NA SHALKE O4 ZOTE ZIMEFUZU KATIKA KUNDI G HUKU FC PORTO IKISHIKA USUKANI WA KUNDI H IKIFUATIWA NA SHAKTAR DONESTSK NA KUFANIKIWA KUFUZU KWENYE MTOANO WA 16 BORA
LIGI KUU YA UINGEREZA IJULIKANAYO KAMA BARCLAYS PREMIUM LEAGUE IMEFANIKIWA KUPITISHA TIMU 4 KATIKA AWAMU HIYO YA MTOANO AMBAZO NI MANCHESTER UNITED, CHELSEA, ARSENAL NA MANCHESTER CITY