Thursday 11 July 2013

MSANII LULU, ATWAA TUZO YA MSANII BORA WA KIKE ZIFF 2013


MSANII wa filamu mwenye misukosuko nchini Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' amefanikiwa kutwaa tuzo ya msanii bora wa kike wa mwaka kwenye tuzo za Filamu za Kimataifa za Nchi za Majahazi lijulikanalo kama ZIFF.

Lulu amenyakua taji hilo kwenye kipengele cha filamu za Kitanzania ijulikanacho kama Tuzo za Zuku swahili Bongo Movie kwa msanii bora wa kike wa mwaka kufuatia kuwika vizuri kwenye filamu ya 'Women of Principles' iliyochezwa na mastaa kibao akiwemo Ray Kigosi ambaye pia ndio muongozaji mkuu wa filamu hiyo.
Wengine Nargus Mohamed aliyekuwa miss Tanzania, Caesar Daniel mtangazaji maarufu wa Bongo star search na wengine wengi ambayo ndani ya filamu hiyo iliyochezwa na kuelezea usaliti kwenye ndoa.
Kwa tuzo hiyo ya msanii bora wa mwaka Lulu anakuwa msanii wa kwanza mwenye umri mdogo kunyakua tuzo hiyo yenye heshima kubwa Duniani kwa sasa kufuatia majaji wanaochagua washindi kutoka nchi mbalimbali.   
Wengine waliokwisha wahi kunyakua tuzo hiyo ni pamoja na Iyvon Shelly 'Monalisa', Baby Madaa ambapo wote walitwaa tuzo hiyo kwa mwaka tofautitofauti.
Hata hivyo katika tuzo hiyo Lulu hakuwepo na tuzo yake kupokelewa na mwakilishi wake, aidha kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alipokea kwa furaha ushindi huo na kumshukuru Mungu.
Aidha, kwa upande wa filamu ya Bond Bin Suleman "Lovers Islands" ilifanikiwa kuwa filamu bora ya kiswahili ya mwaka huku mtunzi wake Javed Jafferji akiibuka pia muongozaji bora.
kwa upande wa tuzo maalum ya Bi Kidude ilikwenda kwa filamu ya 'Crush '(HUSUDU)' iliyotengenezwa na Issa Mbura ambaye ni msomi wa sanaa chuo kikuu cha UDSM.
Tuzo bora ya Afrika Mashariki ilikwenda kwa filamu ya 'Half Nairobi', huku tuzo ya Golden Dhow ilikwenda kwa filamu ya 'Golchehreh'.
Filamu zingine zilizonyakua tuzo za ZIFF 2013' pamoja na Shoeshine ya Amil Shivji (Tanzania), Fluorescent sin (Kenya), Ni sisi (Kenya)' na nyingine nyingi.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako