Wednesday 31 July 2013

MTIHANI WA UWAKALA WA FIFA KUFANYIKA TANZANIA.


MTIHANI wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.
MSEAMAJI WA TFF BONFACE WAMBURA

Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.
KUSHOTO NI SAID TULI MMOJA KATI YA MAWAKALA WANNE WA TANZANIA WANAOTAMBULIWA NA FIFA.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako