Friday 19 July 2013

SAFARI YA JOVETIC KUTUA MAN CITY

Stevan Jovertic akiwa kazini




Klabu ya Serie A ya Fiorentina yathibitisha  kufikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wao Stevan Jovetic kwenda  Manchester City.
Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Montenegro mwenye umri wa miaka 23, aliyekuwa moto wa kuotea mbali katika msimu uliopita aliweza kuifungia timu yake mabao 13 katika mechi 31 mwisho mwa msimu uliopita,amekuwa akiwaniawa na timu kubwa zikiwemo  Manchester United, Chelsea na Arsenal.
Taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya  Twitter ya Fiorentina inasema: "makubaliano kufikiwa na Klabu ya soka ya Manchester City  kwa ajili ya kumnunua mchezaji Stevan Jovetic."
Man City tayari imeshajiimarisha kikosi chake kwa  kuongeza kiungo Fernandinho kutoka Shakhtar Donetsk  winga Yesu Navas kutoka Sevilla, na kutarajia kumsajili mchezajiAlvaro Negredo  siku zijazo kuweza kuziba pengo la Mario Balotelli na Carlos Terves.
Jovetic, ambaye anaweza kucheza kama kama mshambuliaji binafsi, ama mbele ya kiungo, alifunga bao lake la 10 kwa ajili ya taifa lake katika mechi ya kirafiki dhidi ya Latvia mwisho Agosti.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako