Sunday 21 July 2013

MECHI ZA KUJIANDAA NA MSIMU: MANCHESTER ILIVYOIVURUMISHA ALL STAR YA SYDNEY

DAVID MOYES amepata ushindi wake wa kwanza katika mchezo dhidi ya A league all Star kwa mabao 5-1, ikiwashuhudia makinda wake Danny Welbeck na Jesse Lingard katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu ujao.
WELBECK AKIFUNGA MOJA YA MAGOLI YAKE
KINDA LINDAGARD ANAYEKUJA KWA KASI KATIKA KIKOSI HICHO CHA MANCHESTER UNITED
MOYES NA MAJUKUMU MAPYA ANAANZA KULA MATUNDA YA UKIOCHA SASA
Michezo hiyo ambayo ni maalumu kwa nia ya kujijenga kibiashara na kuwajengea uzoefu wachezaji wachanga imemfanya kocha David Moyes kuona ipo haja ya kukaa na mchezaji wake Danny Welbeck kuongea nae ili kumuongezea ujuzi anapokuwa karibu na goli.
MANCHESTER UNITED WAKISHANGILIA MOJA YA MAGOLI YAO
Akiwa amefunga magoli mawili msimu uliopita Welbeck anaonekana mwenye uchu na mabadiliko makubwa anapokuwa analikaribia lango la wapinzani.
VAN MAGOLI NAE ALIKUWEPO KATIKA KUZIFUMANIA NYAVU ZA WAPINZANI
Katika mchezo huo Mabao ya Manchester yalifungwa na mshambuliaji kinda Jesse Lingard mabao mawili, Dany Welbeck mabao mawili na Robin Van Persie.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako