Thursday 25 July 2013

COASTAL UNION WALIVYOWAANGAMIZA URA NDANI MKWAKWANI.


KIKOSI cha Coastal Union maarufu kama Wagosi wa kaya kutoka jijiniTanga waliweza kuvunja  mfupa uluiomshinda fisi baada ya kuwanyuka timu ya mamlaka ya kukusanya mapato URA, kwa bao moja lililofungwa na winga Keneth Masumbuko Na kuifanya timu hiyo kuibuka kidedea katika mchezo huo.

TAMMIM KAZIN

Pamoja na Coastal kuonekana kutawala mchezo huo lakini mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyoona mlango wa mwenzake.
MASHABIKI NA WALIKUWEPO KUTOA SAPOTI KWA TIMU YAO


Kipindi cha pili kilanza kwa kasi lakini alikuwa ni Kiungo hatari wa Coastal Union aliyesajiliwa kutika timu iliyoshuka daraja yaPolisi Morogoroaliyeifungia timu yake bao safi na kufanya mpaka mchezo unamalizika timu ya Coastal union kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

UHURU SULEIMAN AKIFANYA MAMBO YAKE UWANJANI HAPO

Suala la Coastal Union kuvaa jezi nyeupe kipindi cha kwanza na nyekundu kipindi cha pili ni kutokana na makosa katika pre match meeting ambapo hawakuafikiana kuhusu rangi za sox, ikaonekana sox pamoja na fulana zinafanana kwa mbaali. coastal Union kwakuwa ni wenyeji walilazimika kubadili jezi zao na kuvaa rangi nyekundu kataaika iipindi cha pili kama utakuwa makini utaona kuna jezi nyeupe na nyekundu, usiogope.


UHURU ALIKUWA HAWEZEKANI HAPO

LAZIMA MTU AFUNGWE HAPA
KINDA ABDI BANDA AKIFANYA MAMBLO YAKE

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako