Tuesday 23 June 2015

KWENYE MSIBA WA FLORENCE DYAULI MTANGAZAJI WA TBC




























AJALI BARABARANI

Moja ya Ajali tulizokutana nazo maeneo ya Moroco asubuhi hii wakati tukielekea kumpumzisha Bi Florence Dyauli mwandishi wasiku nyingi wa Tbc
Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa ya mtu kopeteza maisha ila ni majeruhi waliokimbizwa hospitali ya karibu
Mungu atulinde na ajali na atufishe pale unapofika wakati wa mtu kurudi kwake.

Friday 15 May 2015

HAPPY LOVELY BIRTHDAY DAVID DAVE HOLLELA

Happy birthday to you buddy wishing you happiest life and enjoy your day
God bless you...!

Thursday 14 May 2015

PIC OF THE DAY

Everything Is Possible Under the Sun

HAPPY BIRTHDAY MAMA YETU MAMA SAADA

Imekuwa ni siku njema kwako Allah akujaalie kheri uishi miaka mingi maisha yenye furaha amani na upendo....!
Happy Lovely birthday Twalhiya

Better Muzic

For The Better Muzic Join with NURUMUZIC Production

FAINALI UEFA JUNI 6, NI KATI YA FC BARCELONA VS JUVENTUS


Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa UEFA itafanyika Juni 6, 2015 kwa kuwakutanisha Mabingwa wa Hispania klabu ya Fc Barcelona dhidi ya Wazee wa Turin Juventus katika uwanja wa Olympiastadion, Berlin nchini Ujerumani
Barca waliwatoa Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali kwa jumla ya Goli 5-3
Wakati Juventus wamefanikiwa kutinga fainali hizo baada ya kuwaliza Real madrid kwa jumla ya goli 3-2

HALI TETE NCHINI BURUNDI KWA RAIS NKURUNZINZA

Raisi Pierre Nkurunzinza
Tukiangazia hali ya mambo nchini Burundi aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano hii  kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.
Hayo yanajiri wakati Rais Pierre Nkurunziza anashiriki mkutano wa kikanda wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Burundi.
Burundi imekua ikishuhudia maandamano ya raia wakipinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza. Kwa muda wa majuma kadhaa mitandao ya kijamii, na vyombo mbali mbali vya habari vimekuwa vikiripoti taarifa hizo kutoka huko Burundi
Mpaka sasa haijajulikana kundi gani lina mamlaka ya uongozi wa nchi, baada ya kundi la wanajeshi linaloongozwa na jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kuipindua serikali ya Pierre Nkurunziza.
Hata hivyo Ikulu ya rais huyo imeendelea kutangaza kupitia akaunti yake ya twitter kuwa mapinduzi hayo yamefeli, baada ya jeshi kuingilia kati na kudhibiti hali ya mambo.
Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita vimezuka karibu na afisi za kituo hicho cha habari.Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo la kukiteka kituo hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu na watutsi; vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa nchini humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa. lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi jirani ya Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa na masuala ya ukabila.
Rais Piere Nkurunzinza alizaliwa desemba 18/1963 mjini Bujumbura katika familia ya wahutu

Na baba yake Yustach Ngabisha alikuwa mbunge wa Burundi mwaka 1965 aliuwawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka1972
Jenerali Godefroid Niyombare
Meja Jenerali Niyombare ambae ndie ametangaza mapinduzi hayo nchini Burundi, aliteuliwa kuwa kamanda mkuu wa jeshi la Burundi mwaka 2014  akichukua nafasi ya Adolphe Nshimirimana akiwa anatokea nchini Kenya kama balozi wa Burundi
Lakini alitumuliwa na Nkurunzinza kama mkuu wa usalama February 2015 bila kutolewa sababu za uamuzi huo
Umoja wa mataifa umeonya hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa Burundi itakuwa na Amani na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo itarejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe .
watu zaidi ya 20 wameuawa tangu tarehe 25 mwezi uliopita baada ya Nkurunzinza kutangaza kuwania muhula wa tatu madarakani kinyume na katiba ya taifa hilo ambayo inaruhusu mihula miwili tu ya miaka mitano kila mmoja akidai muhula wake wa kwanza alichaguliwa na bunge na wala sio wananchi. Zaidi ya waburundi 50,000 wametorokea nchi jirani kufuatia ghasia za kabla ya uchaguzi wa mwaka huu
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limeitisha kikao cha dharura kujadili hali ya mambo Burundi baada ya jenerali mwandamizi jeshini kutangaza kunyakua madaraka kutoka kwa Rais Pierre Nkurunziza. Kikao hicho cha dharura kimeitishwa na Ufaransa  huku katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa wito wa utulivu na ustahamilivu nchini Burundi. Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu kinachoendelea nchini Burundi na kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu Ban Ki-moon aliyotoa wakati wa mkutano wa viongozi wa umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia kuhusu awamu za uongozi.
Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric aliyezungumza mjini New York, wakati wa mkutano na waandishi wa habari waliotaka kufahamu msimamo wa chombo hicho kuhusu hali iliyoripotiwa nchini Burundi.

Wednesday 15 April 2015

MECHI ZA UEFA HATUA YA MTOANO ROBO FAINALI-------------

Katika Jiji la Madrid huko uhispania kulikuwa hapatoshi katika mchezo uliowakutanisha Miamba ya jiji hilo, Atletico Madrid na Real Madrid ambazo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya, hatua ya robo fainali.
Atletico waliowakaribisha Real katika mchezo uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon, ambapo timu hizo zitarudiana katika uwanja wa Santiago Bernabeu tarehe 22 Aprili.
mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak alikuwa kikwazo kwa real, ambaye alinga'ara katika mchezo huo kwa kupangua michomo mikali kadhaa ya wachezaji wa Real Madrid walokuwa wakilisakama lango la atletico, huku Mario Suarez wa Atletico Madrid akikosa nafasi ya kuifungia timu yake mwishoni mwa mchezo huo.
Naye winga Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale aliyekosa nafasi muhimu mapema katika dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza cha mchezo kwa kushindwa kutumbukiza mpira wavuni amesema walistahili kushinda, ingawa haikuwa hivyo.
 “NI MATOKEO MAZURI KUENDEA HATUA YA MARUDIANO KWA SABABU HATUKURUHUSU GOLI LOLOTE. KWA UPANDE WANGU NAFKIRI TULITAKIWA TUSHINDE, TULISTAHILI KUSHINDA KWA SABABU KIPINDI CHA KWANZA TULICHEZA VIZURI ZAIDI YA ATLETICO BAHATI MBAYA HATUKUWEZA KUENDELEZA KIWANGO KILE KILE KIPINDI CHA PILI”.
Katika mchezo huo Mlinda mlango wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas ameweka historia yake kwa kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi katika michuano hiyo kwa kufikisha michezo 147 akimzidi mchezaji wa Barcelona xavi Hernandez.
Mechi hii jana pia imeweka rekodi kwa Vijana wa Carlo Ancelotti kuwa ni mchezo wao wa saba kukutana na Atletico Madrid bila kushinda.
Mchezo mwingine uliochezwa jana usiku ulizikutanisha timu Juventus ya Italia na Monaco ya Ufaransa, Matokeo ya mchezo huo Juventus iliibuka na ushindi wa goli 1-0. Juventus ilipata bao lake pekee katika dakika ya 57 kwa njia ya penalti ikifungwa na Arturo Vidal.
Hata hivyo kocha wa Monaco Leonardo Jardim, ameilalamikia penalti hiyo kuwa haikuwa ya haki. Timu hizi nazo zitarudiana huko Monaco April 22.
Juventus inalenga pia kufika hatua ya nusu fainali ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.
Wakati huo huo, winger wa monaco Nabil Dirar anaamini mshambuliaji wa timu hiyo aliye kwa mkopo katika timu ya man utd Radamel Falcao atafkiria kurudi Monaco na anatamani asingeondoka Monaco.
Falcao alitimkia man utd kwa mkopo wa muda mrefu lakini amekuwa katika wakati mgumu chini ya van gaal ambaye amekuwa akimuweka benchi.
Mshambuliaji huyo raia wa Colombia amefunga goli nne tu kwa man utd hali inayopelekea utd kusita kulipa kiasi cha pauni milioni 53 ili kumsajili kwa ujumla.
Michezo mingine miwili ngazi ya robo fainali itaendelea leo usiku ikizikutanisha timu ya FC Porto ya Ureno dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, huku Paris Saint Germain ya Ufaransa ikiikaribisha Barcelona ya Hispania.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa aina kutokana na kila timu kuonekana kuwa tishio kwa wapinzani wao.
Timu ya PSG itakosa huduma ya mshambuliaji wake hatari Zlatan Ibrahimovic ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa dhidi ya mechi na Chelsea pamoja na Aurier, kwa upande wa majeruhi watakosa huduma ya Thiago motta pamoja na mlinzi wao david luiz aliye na hati hati ya kucheza.
Kwa upande wa barca wataikosa huduma ya Dani alves pamoja na Thomas vermaelen.
Hata hivyo kocha wa PSG Laurent Blanc amesema hadhani kama falsafa za Barcelona zimebadilika sana na kuongeza kuwa ni kweli wanamiliki mpira vizuri na wana nguvu ingawa na wao wanapenda kumiliki mpira.
Blanc amesema wanaweza kuwafunga barca kwani wao ni moja ya timu chache zilizowahi kuwafunga Barca goli 3.

Thursday 12 February 2015

FAIDA YA TUNDA NANASI



Moja kati ya matunda ambayo yanapendwa zaidi ni tunda la nanasi, linapendwa zaidi kutokana na ladha nzuri na utamu ambao unatokana na sukari iliyoko ndani ya tunda hili ambapo inafanya tunda hili kuwa moja kati ya matunda ambayo yanatumika sana kwa kutengeneza juice.

Hata hivyo baada ya kusoma taarifa hii ya utafiti utapata sababu zaidi za kupenda kula mananasi, zipo faida nyingi sana kwenye mwili wa mwanadamu faida ambazo ni za kiafya zaidi.

Mananasi yana virutubisho hivi muhimu kwa mwili wa mwanadamu.
Mananasi ni chanzo muhimu sana cha vitamin pamoja na madini ambayo yanasaidia kuimarisha afya ya mwanadamu ambazo ni kama vile Thiamin, Riboflavin, Vitamini B-6 , Folate , Acid ya Pantothetic pamoja na madini ya Magnesium, manganese na potasia.
Katika hesabu za kitabibu, kipande kimoja cha nanasi kinatosha kuongeza 131% yavitamin c ambayo mwili wako unaihitaji kwa siku moja.

Mananasi husaidia kutibu vidonda na uvimbe.
Moja kati ya vurutubisho vilivyoko ndani ya nanasi kinaitwa Bromelain, husaidia sana kuondoa maumivu kwenye viungo, kupunguza hali ya uvimbe kwenye tezi  na hata kupunguza uvimbe wa kawaida ambao umetokea ndani ya mwili na pia humsaidia sana mtu akiwa amefanyiwa upasuaji.

Mananasi husaidia Mfumo wa usagaji (Mmeng’enyo) wa chakula.
Manansi yana virutubisho vya kambakamba (fibre) ambavyo husaidia sana kwenye kusagwa kwa chakula mwilini, kirutubisho cha Bromelain pia husaidia kwneye kusaga chakula tumboni kwa kusaidia kuvunja vile vipande vya protini.
Manufaa ya nanasi kwenye ngozi
Vitamini C ipatikanayo kwenye mananasi husaidia sana kuipa ngozi mng’ao ambao unahitajika, mishipa midogo ya damu pia hufaidika sana kutokana na mananasi pamoja na viungo vingine vya mwili na mifupa pia.

Manufaa ya nanasi kwenye mifupa
Mananasi yana madini aina ya Manganese ambayo husaidia kuzalisha nishati mwilini huku ikisaidia kutoa ulinzi kwa seli za mwili wa mwanadamu.
Madini haya yanasaidia sana ufanyaji kazi wa madini mengine na virutbisho kamaThiamine na Biotin ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia kufanya mifupa kuwa migumu na yenye afya zaidi na pia husaidia kuyayusha vyakula vyenye mafuta.

Mananasi husaidia Macho .
Tunda aina ya nanasi lina vitamin A pamoja jna kirutubisho aina ya Beta-Caroteneambavyo kwa pamoja husaidia mfumo wa kinga ya mwili na afya ya macho.
 Mananasi hutoa nguvu na nishati na kushusha shinikizo la damu.
Mananasi ya kiwango kikubwa cha Vitamini B1 na B6 ambavyo ni vyanzo muhimu sana vya nishati pamoja na kuvunjavunja sukari kwenye mfumo wa usagaji wa chakula.
Madini ya shaba pia yanapatikana kwenye mananasi yanasaidia sana kutoa afya kwa seli nyekundu zinazosaidia kutengeneza damu na madini ya potasia ambayo yanasaidia kuweka mapigo ya moyo sawa na kushusha shinikizo la damu.

Monday 9 February 2015

HONGERA IVORY COAST KWAKUWA MABINGWA WAPYA WA AFCON


Timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast imefanikiwa kuunyakua ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa mara ya pili, baada ya kuibwaga Ghana 'Black Stars' katika mechi ya fainali iliyochezwa nchini Equatorial Guinea. Kwenye pambano hilo kali na la kusisimua  lilimalizika katika dakika 90 za mchezo, huku timu zote mbili zikitoka sare ya bila ya kufungana.
 Muda wa dakika 30 za nyongeza nao haukuweza kumtoa mshindi wa pambano hilo. Baada ya kumalizika dakika 120 za mchezo, ulichukuliwa uamuzi wa kupigiana penalti  tano – tano, na hapo ikajirudia historia ya fainali ya mwaka 1992.
 Ivory Coast ilianza kupoteza penalti zake mbili, huku Ghana wakiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi, lakini Ivory Coast ilianza kujirekebisha katika upigaji wa penalti, na Ghana nao wakaharibu mikwaju yao miwili, lakini baada ya kuendelea michomo ya funga nikufunge, hatimaye kipa wa Ivory Coast alizuia mkwaju wa kipa wa Ghana, na kutandika mkwaju wa tisa na kuibeba Ivory Coast kwa ushindi wa mabao 9-8.
Mchuano huo ulirejesha historia ya fainali ya mwaka 1992, ambapo Ivory Coast iliutwaa ubingwa huo kwa kuifunga Ghana kwa mikwaju ya penalti 12 kwa 11. Ghana imeshalinyakua kombe la mataifa ya Afrika mara tano. Siku ya Jumamosi, ilichezwa mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo kati ya wenyeji Equatorial Guinea ilipokamuana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Kongo ilishinda kwa penalti 4-2.