Friday, 26 July 2013

KIKWETE APEWA JEZI YA MESSI


Rais Jakaya Kikwete azawadiwa jezi yenye Jina lake ya Timu ya Barcelona ikiwa na namba 10 mgongoni.
BIA ya Castle Lager imeingia makubaliano ya kuidhamini moja ya klabu maarufu zaidi duniani ya FC Barcelona ya Hispania kwa kipindi cha miaka mitatu udhamini utakaokifanya kinywaji hicho kuwa bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika.

Ushirikiano huu, uliyosainiwa kwenye uwanja wa klabu Camp Nou, unaifanya CASTLE Lager kuwa bia rasmi itakayotumika kwa shughuli yoyote ambayo Barcelona itashiriki kwenye bara la Afrika na pia itafungua milango kwa mashabiki wa Barcelona Afrika kuwa karibu na wachezaji wa Barcelona, vifaa, na kumbukumbu. Pia kupata nafasi ya kusafiri kwenda Hispania kushuhudia kwa karibu timu ya Barcelona.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas akikabidhiwa jezi kwa ajili ya Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Javier Faus, ambaye ni Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia uchumi huko Catalonia Hispania leo hii baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona.
Mkataba huu utakuwa maalum kwa ajili ya CASTLE Lager kwenye nchi nyingi za Afrika isipokuwa kwa baadhi ya nchi chache zilizochaguliwa ambapo itatumika Castle Milk Stout.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya bara la Afrika. Kushirikiana na bia bingwa Afrika litaongeza kwa haraka umaarufu wa timu ya FC Barcelona ndani ya bara la Afrika na kufungua milango kwa mashabiki wa klabu hii kupata bidhaa mbalimbali za Barcelona na nafasi za kushinda safari ya kwenda Barcelona kuitembelea klabu hiyo.
NEYMAR AND MESSI
“Tumefurahi sana kuingia katika ushirikiano na Castle Lager na Castle Milk Stout, chapa zinayofahamika dunia nzima . Tunafanana na Castle kwa kuwa sote tuna historia ya zaidi ya miaka 100 na utamaduni uliotukuka. Na sote tuna mapenzi na mpira wa miguu pamoja na mashabiki wake katika soko muhimu kama Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia masuala ya uchumi.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako