Sunday 30 June 2013

KAMBI YA KINA MBWANA SAMMATA YAKUMBWA NA BALAA GHANA

Kambi ya waliowahi kuwa mabingwa wa soka wa Afrika timu ya Tp Mazembe imekumbwa na balaa mara baada ya Nahodha wake Tresor Mputu kufiwa na mmoja wa kaka zake wakubwa aitwaye Ndombele maarufu kwa jina la Weah.
Wachezaji wa timu hiyo  akiwemo mtanzania Mbwana Sammata na Thomas Ulimwengu wapo Ghana kwa ajili ya mashindano ya ligi ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Hearts of Oak.walikusanyika zaidi ya saa moja katika chumba cha kiungo huyo kumfariji kabla ya uongozi haujapitisha uamuzi wa kumrudisha Congo kujumuika na ndugu zake katika msiba huo,.
Weah ambaye ni kaka wa mchezaji huyo alifariki tarehe 29 jumamosi hii mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.
TRESOR MPUTU NAHODHA WA TP MAZEMBE

UKWELI WA HABARI ZA THIAGO ALCANTARA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED


KLABU ya Mashetani wekundu Manchester United imetuma ofa ya Paundi million 18 kuhakikisha inamsajili kliungo   Thiago Alcantara wa timu ya FC BARCELONA aweze kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa mwaka 2013-2014.
Kama dili hillo litakamilika Thiago atakuwa anatia kibindoni mara tatu ya mshahara  aliokuwa akipokea katika timu ya Barcelona na atakuwa akipokea paund 140,000. Kwa wiki na  kumfanya  kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa wanalipwa pesa ndefu katika timu hiyo.
Chanzo cha kuaminika cha mchezaji huyo kilisema Thiago anajiandaa kuongea na viongiozi wa Barca juu ya ombi lake la kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho cha wakatalunya huku raisi wantimu hiyo akiwa na matumaini ya kumbakisha mchezaji huyo mara baada ya kuongea na mzazi wa Thiago aitwaye Mazinho.
Thiago aliwahi kusema huko mwanzo kutorizishwa na klabu hiyo haswa kutokana na kushindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza game nyingi zaidi na hivyo kufanya samani yake kushuka kwa kiasi kikubwa.
Kama dili lake litakamilika Thiago atakuwa anapokea mshahara mkubwa zaidi ya Shinji kagawa,Dany welbeck, na Phil jones wanaolipwa paundi 810,000 kwa wiki.
THIAGO AKIWA NA JEZI YA TIMU YA VIJANA YA SPAIN ILIYOCHUKUWA UBINGWA WA ULAYA

THIAGO AKIWA NA JEZI YA MAN UNITED LAKINI SI PICHA HALISI

KUNGO HATARI THIAGO ALCANTARA AKIWA NA KOTI LA TIMU YAKE YA FC BARCELONA

Saturday 29 June 2013

AJALI MBAYA YA GARI LA WATALII NCHINI UGANDA

LORI LA WATALII LIKIWA LIMEHARIBIKA VIBAYA MARA BAADA YA AJALI

WANANCHI WAKILISHUHUDIA GARI LA MAZIWA LILILOSABABISHA AJAL HIYO LIKIWA LIMEHARIBIKA VIBAYA
WANANCHI WAKILISHANGAA GARI HILO MARA BAADA YA AJALI
Lori lililobeba watalii nchini Uganda katika kitongoji maarufu kwa jina la Nabunsake kilomita chache kufika katika mji mkuu kampala lilipinduka na kusbabisha vifo vya watu watatu
WATAFUTA CHOCHOTE NAO WALIKUWEPO
.
Shuhuda wa tukio hilo alisema chanzo cha ajali hiyo kilisababishwa na lori la maziwa lililokuwa katika mwendo kasi na kuipita cruiser(aina ya gari) bila ya umakini.

GARI MRA BAADA YA AJALI MBAYA
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali nyingi zinazotokea katika barabara hiyo zimuwa zikisababishwa na malori hayo ya maziwa yanayoendeshwa kwa mwendo kasi na bila umakini na hivyo kuwataka polisi kuwa makini na maisha ya watu na si manufaa ya mabosi wa magari hayo ya maziwa.

CHEICK TIOTE WA NEWCASTLE AKUBALI KUVAA JEZI ZENYE NEMBO YA KAMPUNI YA MICHEZO YA KAMARI CISSE AKIENDELEA KUWEKA NGUMU.

MCHEZAJI WA NEWCASTLE HATIM BEN ARFA AKIWA KATIKA POZI NA JEZI ZA WONGA
lile sakata linalowahusu wachezaji waumini wa dini ya kiislamu wa timu ya Newcastle kugoma kuvaa jezi za wazamini wapya wa timu hiyo zenye nembo ya neno WONGA limechukua sura mpya mara baada ya baadhi yao wakionekana kulegeza maamuzi yao na kuanza kukubali kufanya hivyo.
PAPIC DEMBA CISSE AKISHANGILIA MOJA YA MAGOLI ALIYOIFUNGIA NEWCASTLE AKIWA NA UZI WA MZAMINI WA ZAMANI
Habar zilizothibitishwa bna gazet la Daily Mirror la uingereza liomeripoti kuwa mchezaji Cheick Tiote ameshakubali kuvaa jezi yenye nembo hiyo na hivyo msimu ujao ataonekana akiwa ndani ya uzi wenye nembo ya wonga lakini tatizo lipo kwa Papis demba Cisse ambaye bado wanafanya nae mazungumzo.
Wonga bambayo ni kampuni inayohusika na michezo ya bahati nasibu maarufu kama kubet inaenda kinyume na sheria za dini ya kiislamu na wachezaji wa Newcastle Hatim Ben Arfa, Cheick Tiote na Papic Demba Cisse hawakuwa tayar kufanya hivo mchezaji ingawa Ben Arfa alishakubali na kufanya matangazo ya jezi hizo mpya.
MCHEZAJI CHEICK TIOTE MIONGONIO MWA WACHEZAJI WENYE ITIKADI YA KIISLAMU AKIFANYA VITU VYAKE NA TIMU YAKE YA NEWCASTLE

Friday 28 June 2013

AFRICA YA KUSINI WAKESHA KUMUOMBEA MADIBA MANDELA


                                              Nelson Madiba Mandela

Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.

Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.

Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.

NEY Ft DIAMOND NDANI YA NEW MAISHA CLUB

 
Msanii wa Muziki wa HIP HOP Ney akiwa sambamba na Msanii wa Bongoflava Diamond wakiimba track ya Muziki Gani ndani ya New Maisha Club hivi Karibuni. 

VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)

 


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)


VIDEO - PENALTI NUSU FAINALI (HISPANIA Vs ITALY)

 
 

Thursday 27 June 2013

STAILI MPYA YA NYWELE ZA RAHEEM STERLING WA LIVERPOOOL MSIMU UJAO

Raheem Sterling na stail ya zaman ya nywele

Sterling akimpeleka puta Arteta wa Arsenal na stail ya nywele ya zaman lkn ya kuvutia
Sterling akiwa kazin na timu ya vijana ya England
 STAILI MPYA ALIOKUJA NAYO RAHEEM STERLING KINDA LA LIVERPOOL
Sterling ndani ya staili mpya ya nywele
Sterling akijiandaa kwa msimu ujao na stail ya kustaajabisha ya nywele zake
Raheem Sterling ndani ya mazoez na mkato mpya wa nywele sijui tutauita jina gani?


BRAZIL ILIPOILAZA URUGUAY KWA 2-1

Brazil imeifunga uruguay mabao 2-1 katika mchezo uliozikutanisha timu hizo, magoli ya Brazil yalifungwa na Fred na Paulinho wakati lile la Uruguay likiwekwa kimiani na Edison Cavan.
Mchezaji wa Brazil Fred akishangilia bao la kwanza la Timu hiyo akiwa na wenzake Hulk(19) na   Dan Alves (2)
Mchezaji wa Brazil Neymar akifanya vitu vyake
Neymar akiwasumbua  Uruguay, kona ya Mchezaji huyo ndio iliyozaa bao la pili
Mlinda mlango wa Brazil Julio cesar akiokoa penat ya uruguay iliyopigwa na  Diego Forlan mara baada ya David luiz kmsukuma mchezaj wa urugua katika eneo la hatari
Wazee wa Samba wakiwaaga mashabiki wao mara baada ya kwisha kwa mchezo huo
THIAGO SILVA NA FRED  WAKIMPONGEZA KIPA WAO JULIO CEASER BAADA YA KUOKOA PENALT YA FORLAN
FRED AKITUPIA GOLI LA KWANZA KWA BRAZIL

Wednesday 26 June 2013

HABARI MPYA INAYOMHUSU RONALDO KURUDI MANCHESTER IKO HAPA

Ronaldo akiwa na Mzee wa Ferguson katika mechi iliyowakutanisha Manchester na Real Madrid

Mshambuliaji wa Real Madrid Christian Ronaldo anajiandaa kuongea na klabu yake ya zamani ya Manchester United juu ya mustakabali wake wa kusajiliwa na timu hiyo ya jiji la Manchester United.
Kocha mpya wa Man united David Moyes
Gazeti la michezo la Daily Mirror la uingereza limetoa taarifa kuwa mchezaji huyo aliye mapumnzikoni ana asilimia chache za kuendelea kubaki Santiago Bernabeu kwa mara nyingine  na vikao vya siri kati ya mchezaji huyo na mashushu wa klabu ya manchester United  inaweza kuwa ndo chanzo cha mchezaji huyo kuwa karibu kurudi katika jiji la Manchester United.
Ronaldo enzi zake akiwa Man united
Madrid walikuwa na matumaini ya kumbakisha mchezaji huyo haswa kocha wake mpya Carlo Anceloti alipotoa taarifa kuwa anajisikia faraja xana kufanya kazi na mchezaji huyo na taarifa za kubaki kwa wayne rooney katika klabu hiyo kunatoa mwanya kwa timu hiyo kuweza kujiimarisha msimu ujao.
Ronaldo akifanya vitu vyake Madrid

Tuesday 25 June 2013

SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA POLISI KUMNANIHII MDADA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA

Ilikuwa Juni 18, mwaka huu katika Uwanja wa Soweto wanachama na wapenzi wa CHADEMA walikukusanyika ili kuwaaga watu wanne waliokufa kufuatia bomu lililolipuka Juni 15, katika uwanja huo.
Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini humo alifika uwanjani hapo kumwokoa baba yake Godwin Malisa ambaye ni mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha mbwa mwizi....Anaendelea kusema: “Nilimwambia baba tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa... ..Askari mmoja akasema ‘laleni chini’, tukalala tukidhani tutakuwa salama. Lakini walikuja askari na kutupiga marungu mwili mzima mimi na baba,... ” Mara wakatokea askari wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga mpaka mkono na mguu ya kushoto ikavunjika.
“Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba wakati askari wanatupiga. Askari mmoja alirarua gauni langu chini na juu, hadi nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya mapaja yangu ili alipue sehemu za siri, wenzake wakamkataza. Mwingine alisema kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia akasema watuue wote, mimi niliomba wasituue maana nimeacha mtoto mchanga nyumbani.”
Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama wa Chadema.
“Walisema ‘unajifanya wewe Chadema, sasa ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea CCM wewe.’ Mimi niliwaambia sina chama chochote nimekuja kumwokoa baba yangu. Wakati huo wote walishanivua hereni, simu wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.”
“Kisha likaja gari la polisi tukabebwa na kuingizwa humo. Mwendo tuliondoka pale ulikuwa wa kasi huku wakiendelea kulipua mabomu na kutukanyaga bila kujali. Tulishtukia tuko Hospitali ya Mount Meru, tukabwagwa hapo na gari hilo likaondoka.”

Chanzo: Mwananchi - Juni 24 2013

MANCHESTER UNITED KUMSAJILI CAVAN.

Picha ikimuonesha Cavan atakavyokuwa anaonekana akiwa na jezi ya Man united(si picha halisi)
Klabu ya Manchester united iko tayari kutoa ofa ya paundi millioni 50 kwa  Napol  kumsajili mshambuliaji Edison Cavan aweze kujiunga na Mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester.
Rafiki wa nyavu Cavan akishangilia moja ya mabao aliyoifungia Napol
Habar zilizoandikwa na gazeti la Daily Mirror zinasema familia ya Glazzer inayomiliki timu ya Manchester United iko tayari kumpa David Moyes kitita cha paundi millioni 50 ili iweze kushinda vita ya baadhi ya klabu kubwa zinazomuwania mchezaji huyo zikiwemo Madrid na Manchester City.
Akiwa na uzi wa mazoez wa Napol
Moyes anatafuta mtu atakayekuwa pacha wa Robin Van Persie katika safu ya ushambuliaji na uchezaji wa nguvu na akili za kufunga mabao ndizo zilizomvutia David Moyes ingawa Napol wanaweza kukataa ofa hiyo kwani walishatangaza dau la mchezaji huyo ni paundi million 54
hivyo kama Manchester wanamtaka itabidi waongeze kitiota hicho.

MCHEZO HATARI WA BINADAMU NA NG'OMBE

Mcheza michezo ya kuwachokoza ng'ombe akichotwa na pembe baada ya kumkasirisha mnyama huyo

Hii ndo hatari zaid anaweza kukusababisha usipate choo


Rafael Cerro mcheza michezo ya kuchokoza N'gombe akiwa ameshika kisu kwa madhumuni ya kumchokoza mnyama huyo na akishamshinda ujanja anamchinja na kufanywa kitoweo...... shauri yako kama umezoea michezo ya kukimbiza kuku Je N'GOMBE UTAWEZA?

PICHA ZA SAMATTA AKIWA KAZINI MECHI YA TP-MAZEMBE NA LUPOPO ZIPO HAPA

Mbwana samatta a.k.a "Samagoals aliyevaa nambari 15," akivizia mpira wa kona katika goli la Fc Lupopo
Hekaheka langoni kwa FC lupopo
Samatta na wachezaji wenzake wakimpongeza mcheaji mwenzao mara baada ya kufunga bao dhidi ya Lupopo
Mbwana Sammata akifanya mavituzi yake katika mchezo huo ambao Mazembe walishinda bao 1-0,
Kikosi cha Tp mazembe kilichoshinda mchezo huo wa ligi kuu ya Kongo  dhidi ya Fc Lupopo

PICHA ZA MAZISHI YA MAMA YAKE BARNABAS ELIAS

Mama Mzazi Wa Naseeb(DIAMOND) akielekea makaburini Kumzika Mama wa Msanii Barnabas Elias (Bi. Mariamu Arubeth)

Mamia ya watu waliofika katika mazishi ya Bi. Mariam Arubeth (Mama yake Barnabas)

Mwili wa marehemu Mariam Arubeth ukiwa ndani ya jeneza kuruhusu heshima za mwisho

Msanii Barnabas akishikiliwa kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa Mama yake Mzazi Bi Mariam Arubeth


Barnabas Elias Akimuaga mama yake Mzazi Bi. Mariam Arubeth

Barnabas Akijishika kichwa wakati wa kuaga mwili wa mama Yake mzazi


Barnabas akipelekwa kuaga mwili wa mama yake Mzazi Marehemu Mariam Arubeth

Gari iliyobeba Mwili wa Marehemu Mariam Arubeth likiwa tayari kuelekea makaburini

Joh Makini na wananchi Wakitangulia Makaburini kwenda kuuzika mwili wa Marehemu Mariam Arubeth

Baadhi ya wasanii wa THT wakielekea makaburini kusindikiza mwili wa Mama yake Barnabas Marehemu Mariam Arubeth

Wananchi walipokea mwili wa Marehemu Mariam Arubeth kuupeleka makaburini tayari kwa ajili ya mazishi


Mamayake Diamond akimwakilisha mwanae kwenye mazishi ya mama mzazi wa Msanii Barnabas akielekea makaburini akiwa na wananchi wengine.

Baadhi ya wananchi wakisubiri kwenda kuuweka mwili wa Marehemu Mariam Arubeth kwenye makazi yake ya milele

Mamia ya wananchi wakiwa makaburini kusubiri kuzika mwili wa mama yake Barnaas Elias (Marehemu Mariam Arubeth)

Wanafamilia wakitoa maelezo ya kuuweka mwili waMarehemu Mariam Arubeth

Baadhi ya wasanii wakishuhudia tukio la kuweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu mama yake Barnabas (Bi.Mariam Arubeth)

Barnabas Elias Akiweka mchanga kwenye Kaburi la mama yake Marehemu Mariam Arubeth

Baadhi ya ndugu wakimsaidia Barnabas kuweka mchanga kwenye kaburi la mama yake mzazi

Mume waMarehemu akiweka mchanga kwenye kaburi la mke wake Marehemu Mariam Arubeth

Zoezi la kuweka mchanga likiwa linaendelea ndani ya kaburi la marehemu


Barnabas akiwa amepoteza fahamu baada ya kuweka mchanga kwenye kaburi la mama yake mzazi

Barnabas akisaidiwa na wananchi baada ya kupoteza fahamu zaidi ya dakika tano mara baada ya kuweka mchanga kwenye kaburi la mama yake mzazi

Wasanii wakimuingiza Barnabas kwenye gari kumpeleka Hospital mara baada ya kupata fahamu


Umati wa wananchi wakishiriki mazishi ya mama yake Barnabas Marehemu Mariam Arubeth

Mchungaji akiendesha ibada kwenye mazishi ya Mama yake Barnabas

Mume wa marehemu akiweka Msalaba kwenye kaburi la mke wake ambaye ni mama yake Barnabas Elias Mwanamuziki kutoka THT


Ndugu wa Marehemu akisoma Risala kuhusu marehemu Mariam Arubeth Makaburini

Mume wa Marehemu akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Mke wake


Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakiweka Mashada ya maua Kaburini

Kaburi la Marehemu Mariam Arubeth (Mama yake Barnabas Elias)

Mume wa Marehemu akitoa Shukrani wa wananchi walioshiriki Mazishi ya mke wake

Wananchi wakitawanyika mara baada ya mazishi ya Marehemu Mariam Arubeth

PATAPICHA Inawapa Pole Ndugu, Jamaa na marafiki wa Marehemu Bi. Mariamu Arubeth Aliyefariki Dunia Tarehe 22/6/2013. Pia pole zetu za dhati kwa Barnabas Elias, Mume wa Marehemu na ndugu zake wa Karibu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.