Sunday 14 July 2013

LIVERPOOL YAFANYA MAUAJI MECHI ZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA


LIVERPOOL ni hatari ndivyo unavyoweza kusema kwa haraka, wakiwa ndani ya uzi mwekundu wa majogoo wa Anfield Kolo Toure alianza vizuri baada ya timu yake kuibanjua bila huruma timu Preston kwa mabao 4-0.
Alikuwa ni kiungo kinda wa kibrazili Coutinho anayeelezwa kuwa mrithi mpya wa Shuarez alikwamisha mpira kimiani mnamo dakika ya 15 baada ya yeye kuangushwa katika eneo la hatari na kiungo wa zamani wa Liverpool John welsh anayechezea Preston kwa sasa.
Kiungo kinda aitwaye Ibe aliiandikia Liverpool bao la pili katika dakika ya 38 akifumua shuti la umbali wa yadi 20 kutoka golini.
Mchezaji Aspas aliyenunuliwa toka Celta vigo kwa dau la paundi millionio 7.7 aliukwamisha mpira kimiani na kuiandikia Liverpool bao la tatu.
Kama vile alikuwa anawaambia hawakumnunua kimakosa Aspas aliukwamisha mpira nyavuni mnamo dakika ya 75 kuhitimisha karamu ya magoli kwa vijana hao wa Anfield
MCHAWI WA KUZIFUMANIA NYAVU ASPAS AKITUMBUKIZA KIMIANI MOJA YA MAGOLI YAKE KATIKA MCHEZO HUO
ANAYEFANYA VIZURI APEWE HONGERA ZAKE....HAPO COUTINHO AKIPONGEZWA NA JORDAN IBE MARA BAADA YA KUFUNGA BAO LA KUONGOZA
LIVEPOOOOOOOOOOOOOL
 TOURE NDANI YA JEZI YA LIVER KATIKA MCHEZO WA KWANZA NA TIMU HIYO
MTAALAMU COUTINHO AKIPIGA BAO KATIKA MECHI HIYO

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako