YUSSUF AMANI ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA DAMU |
MAHAKAMA ya mkoani Mbeya imehukumu kifungo cha kwenda jela
miaka 30 mkazi wa Isanga Bw Yusuf Aman baada ya kumtia hatiani kwa kosa la
kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 15( jina
linahifadhiwa).
NI AIBU SANA BWANA AMANI AKIJIZIBA SURA KUKWEPA CAMERA ZA WAANDISHI WA HABARI KUPATA SURA YAKE |
Mwendesha mashitaka
wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya
Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo BwYusufu Amani (39) anayedaiwa
kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni
kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya
kuzini.
akisoma Hukumu hiyo
Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye
Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa
miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo
wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito
Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe
taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito
alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa
kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi
wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
KULIA NI MTOTO ALIYEZALISHWA NA BABAAKE AKIWA AMEBEBA MWANAWE HUYO |
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima
Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana
na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana
kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa
kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa
tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa
anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu
kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu
endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo
alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa
kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa
vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa” Na kasha kutoa
hukumu hiyo
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako