Thursday 18 July 2013

UGANDA MJA MZITO AJIFUNGUA MTAANI MARA BAADA YA KUPATWA NA UCHUNGU GHAFLA


MAMA mmoja aliyejulikana kwa jina Generous Atuhire huko nchini Uganda   amejifungua njiani baada ya kuhisi uchungu na hivyo kushindwa kufika hospitalini kwa wakati.

Mwanamke huyo anayeishi katika mji unaojulikana kwa jina la masindi ulioko magharibi mwa Nchi hiyo karibu kabisa na mji mkuu wa Uganda alitokewa na hali hiyo akiwa njiani kuelekea hospitalini hivyo kusababisha wasamaria wema kumsaidia kujifungua mtoto wake huyo .

Generous alieleza kuwa wakati akipata mkasa huo alikuwa njiani na mama ake mdogo kuelekea njiani ndipo alipopatwa na uchungu wa kujifungua.

Ingawa mama huyo aliijifungua salama mtaani na kuwaacha watu wengi wakitaharuki tukio hilo baadae alipelekwa hospitali kwa uangalizi zaidi ambapo daktari  Florence Adoch anayehusika na masuala ya ukunga katika hospitali ya Adochi alisema tukio hilo ni hatari na kuwashauri wajawazito kuwa karibu na vituo vya afya mara wanapokaribia kujifungua.
WASAMARIA WEMA WAKIMSAIDIA GENEROUS KUJIFUNGUA NJIANI MARA BAADA YA KUHISI UCHUNGU WA KUJIFUNGUA. WAJAWAZITO WANASHAURIWA KUWA KARIBU NA MAENEO YA KUJIFUNGULIA MARA WANAPOHISI UCHUNGU

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako